Michuano
ya Ligi ya Taifa inayoshirikisha mabingwa wa mikoa inaanza Mei 27 mwaka
huu katika vituo vitatu tofauti huku Ashanti United ya Ilala na Polisi
ya Mara zikifungua dimba katika Kituo cha Musoma.
Ligi
hiyo ambayo inatarajia kumalizika Juni 12 na 13 mwaka huu itashuhudia
mechi mbili kwa siku katika kila kituo, huku ya kwanza ikichezwa saa 8
mchana na kufuatiwa nay a pili 10 jioni.
Mechi
za ufunguzi Kituo cha Musoma ambapo mechi zake zitachezwa Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma ni Flamingo ya Arusha dhidi ya Forest
ya Kilimanjaro (saa 8 mchana) wakati saa 10 jioni ni Ashanti United na
Polisi.
Kituo
cha Kigoma siku ya ufunguzi kutakuwa na mechi moja tu itakayoanza saa
10 kamili jioni kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika kati ya Mwadui ya
Shinyanga na JKT Kanembwa ya Kigoma. Siku inayofuata ni CDA (Dodoma) vs
Majimaji ya Tabora (saa 8 mchana) na Bandari ya Kagera vs Pamba ya
Mwanza (saa 10 kamili jioni).
Tenende
ya Mbeya na Kurugenzi ya Iringa ndizo zitakazoanza saa 8 mchana kwenye
Kituo cha Mtwara na kufuatia na mechi kati ya Mpanda Stars ya Rukwa na
Ndani ya Mtwara kuanzia saa 10 kamili jioni. Mechi hizo zitachezwa
katika Uwanja wa Umoja.
EEEBWANA HIVI SASA HALI NI MBAYA JUU YA POLISI DHIDI YA RAIA HALI INATISHA NI UNYANYASAJI MTUPU INANIUMA SANA ILA NASHINDWA NA KUNA HAWA POLISI JAMII NA WAGAMBO KAZI YAO KUTESA NA KUCHUKUA RUSHWA KWA RAIA TOA KOMENTI YAKO
ReplyDelete