MO BLOG:
Japhet Kaseba hakuna asiye kufahamu katika ulimwengu wa Tanzania wa
mchezo wa Kick Boxing, hebu tutofautishie kati ya mchezo wa kick boxing
unaocheza na Muay Thai ambayo pia unacheza.
KASEBA:
Unajua kick boxing ni staili ambayo ipo Marekani ambayo inahusisha
ngumi na mateke lakini mateke yake yanaanzia kiononi kuelekea juu, na
Muay Thai ni staili kutoka Thailand ambayo mateke yake yanaanzia kwenye
mapaja kwenda juu.
Pia wanatumia Elbow na kushikana na kudondoshana kitu ambacho kwenye kick boxing hakuna.
MO BLOG: Watanzania wategemee nini maana wewe ndie mwakilishi wetu nje ya nchi.
KASEBA:
Kubwa ni kwamba baada ya kukosa wapinzani kwa muda mrefu katika suala
zima la Kick Boxing nikaamua mimi nijiweke pembeni kidogo na kuamua
kuanzisha ligi ya ‘Bingwa wa Mabingwa’ kwa Tanzania na baadae Afrika
nzima kwa sababu nilikuwa nakusudia kuwaleta washiriki kutoka Japan na
Wanathailend.
MO BLOG: Sasa nini kilitokea na mipango hiyo kukwama..?
KASEBA: Nilikosa udhamini wa kulipia vitu kama sehemu za kulala kwa sababu gharama nyingine walikuwa tayari kujilipia wenyewe.
MO BLOG: Mara ya mwisho tumekujua kama Bingwa wa mchezo wa kick-boxing, lakini ghafla unacheza mchezo wa masumbwi..?
KASEBA:
Kama nilivyosema mwanzo baada ya kukosa mpinzani kwa muda mrefu katika
mchezo wa kick-boxing, niliona ni vyema nikaonyesha kipaji changu katika
mchezo masumbwi. Ndipo nilipopambana na Francis Cheka na mchezo wetu
kuharibika baada ya shabiki kupanda ulingoni.
MO BLOG: Tufafanulie utata uliopo baina yako Francis Cheka katika mchezo wa masumbwi .?.
KASEBA:
Kwa mimi binafsi sidhani kama kuna utata, na kwa sasa najiandaa kwa
pambano la marudiano ambalo nitalitumia kuweka heshima, ambalo
litafanyika tarehe 7 mwezi wa 7 ili kujua nani mshindi wa ukweli.
MO BLOG: Kaseba kuna ukweli wowote kwamba kabla ya kucheza pambano ni vyema siku moja kabla mtu unapaswa kufanya mapenzi.?.
KASEBA:
Kwa kweli kwa kuwa mimi nilianzia kwenye mchezo wa ‘Martial Arts’ ,
hicho kitu kilikuwa kinapingwa sana na sidhani hata katika michezo
mingine kinakubalika. Sana sana ningewaasa watanzania kujituma katika
mazoezi na kuacha kudanganyana.
MO BLOG: Hebu izungumzie familia yako kwa sababu mengi yamesemwa na hatupendi kuyarudia.
KASEBA:
Nampenda sana mke wangu, nawapenda ndugu zangu, pia nawapenda sana
wazazi wangu na siku zote namshukuru mwenyezi mungu na naamini hiyo ni
moja wapo ya mafanikio yangu, kwa kuwa kila ninachohangaikia nahaingikia
kwa sababu ya familia yangu.
MO BLOG: Kumekuwa na taarifa kwamba wewe ni Freemason hebu jitetee.!
KASEBA:
Ee bwana ehh, ha…ha..ha Mo Blog mnanizingua lakini nachoweza kusema ni
kuwa mimi siwezi kukataa wala kukubali na waacheni wanadamu waseme
wanavyotaka, kwa sababu hata Kanumba wamesema ni ‘Freemason ‘ lakini
najua ni ile ‘movie’ aliyocheza ndio imemponza.
Upeo wa watu wengi ni mdogo sana, kwa sababu chochote mtu anachokifanya kwa maana ya kuigiza, watu wengi wanaamini ni kweli.
Ndio maana kuna wanawake wameigiza filamu za uchawi na mpaka leo wanaogopwa mitaani wakionekana kweli ni wachawi.
Kwa
nchi iliyopo chini kama Tanzania ambayo inaibukia kila utakachokifanya
itaonekana ni hivyo hivyo, hata ukiigiza ukasema mimi ni rais ndivyo
baadhi ya watu watakavyoamini.
Mimi ni mkristo ninayependa kumtumikia Mungu.
MO BLOG:
Japhet Kaseba MO BLOG inakutakia mafanikio katika jitihada zako za
kukuza mchezo wa ‘Kick-Boxing’ hapa nchini na katika kufanikisha ligi ya
Masumbwi, na bila kusahau mchezo ujao wa ngumi kati yako na Francis
Cheka; tuko pamoja nawe.
KASEBA: Akhsante sana nami nawatakia kila la heri katika utendaji wenu wa kazi, na msitusahau wanamichezo kama sisi.
No comments:
Post a Comment