Msafara
wa watu 25 wa timu ya Taifa ya wanawake ya Ethiopia umewasili leo (Juni
14 mwaka huu) saa 7 mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines kwa ajili ya
mechi dhidi ya Twiga Stars.
Mechi
hiyo ya marudiano kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Nane za Afrika
kwa Wanawake (AWC) zitakazofanyika Novemba mwaka huu nchini Equatorial
Guinea itachezwa Jumamosi (Juni 16 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Mshindi
baada ya matokeo ya mechi ya awali ambapo Twiga Stars ilifungwa mabao
2-1 na mechi ya Jumamosi atafuzu kwa fainali hizo za Equatorial Guinea.
Nchi ambazo tayari zimefuzu kwa fainali hizo ni wenyeji Equatorial Guinea na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
DRC
ilikuwa icheze raundi ya pili na Equatorial Guinea, lakini baada ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuipa uenyeji Equatorial
Guinea, DRC nayo imefuzu moja kwa moja kucheza hatua hiyo ya fainali.
Makocha
wa Twiga Stars, Charles Boniface Mkwasa na mwenzake wa Ethiopia, kesho
(Juni 15 mwaka huu) saa 5 asubuhi watakuwa na mkutano na waandishi wa
habari kwenye ofisi za TFF kuelezea jinsi timu zao zilivyojiandaa kwa
mechi hiyo.
Viingilio
katika mechi hiyo vitakuwa sh. 10,000 kwa VIP A na sh. 5,000 kwa VIP B
na C. Sehemu nyingine zilizobaki kiingilio ni sh. 2,000 na tiketi
zitauzwa uwanjani siku ya mechi kuanzia saa 3 asubuhi.
No comments:
Post a Comment