Na Mwandishi Wetu
TUZO
za kwanza kabisa za waigizaji wa filamu zimepangwa kufanyika mwezi
ujao, Mratibu wa kampuni ya Bantu Film Award, Stuart Kambona alisema leo.
Kambona
alisema kuwa hatua ya kuanzisha tuzo hizo inatokana na muitikio wa soko
la filamu za Tanzania kwa hivi sasa tofauti na awali. Alisema kuwa
Watanzania wengi walikuwa wanapenda zaidi filamu za kigeni na kufunika
zile za hapa nyumbani.
Alisema
kuwa kutokana na mapinduzi yaliyofanywa na wasanii wa fani hiyo, filamu
za Tanzania kwa sasa zina soko la hali ya juu na imtokana na tabia ya
watanzania kubadili mwelekeo. Alisema kuwa ili kuhakikisha Tanzania
inafikia hatua ya Hollywood, wameamua kutoa tuzo kwa wasanii waliofanya
vizuri na kuifikisha fani hiyo katika hatua ya sasa.
“Tunaamini
kuwa kupitia tuzo hizi, waigizaji au wasanii wa filamu watatengeneza
filamu zenye ubora wa hali ya juu ili kuweza kutwaa tuzo na soko kwa
ujumla, tunaamini tutafikia lengo letu japo tumebakisha muda mfupi mpaka tuzo zenyewe kufanyika,” alisema Kambona.
Alisema
kuwa kwa kuanzia watashindanisha filamu zote za Tanzania ambazo kwa
sasa zipo sokoni ili kutoa fursa kwa kila msanii wa fani hiyo
kushindana. Jumla ya tuzo 28 zitashindaniwa kwa mwaka huu.
Baadhi
ya tuzo hizo ni Filamu Bora, Muongozaji Bora, Muigizani Bora mkuu wa
Kiume, Muigizaji Bora Mkuu wa Kike, Msaidizi Bora Mkuu msaidizi wa kike
na wa kiume, msanii chipukizi bora, filamu ya asili, Mpiga picha bora,
Best Sound Track, Best Make-Up artist, Best Costume Designer, Best
Documentary, Best Visual effect, best Film editor, best script na Tuzo ya Heshima.
Tuzo
nyingine ni Outstanding Pioneer, Best Comedian, Best Cover Design, Best
producer, Best Distributor, Best Action Movie, Best African Film
outside Tanzania, Best Ligting, Best Sound na Best Story.
Muigizaji
nyota wa kike nchini, Irene Uwoya aliwapongeza waandaaji hao kwa
kuanzisha tuzo hizo ambazo alisema zitawapa changamoto kwao kuandaa
filamu za ushindani.
Alishukuru kampuni ya Bantu kwa kuanzisha tuzo hizo ambazo anaamini zitawafanya kuandaa filamu zenye ubora wa hali ya juu.
"Tuzo
hizi zitatufanya tufanye kazi nzuri zaidi ili kuingia katika ushindani,
natoa wito kwa waigizaji wenzangu kufanya kazi kwa umakini ili kuleta
msisimko na ushindani zaidi," alisema Uwoya.
Muigizaji
Mkongwe, Jacob Steven (JB) alisema kuwa anaamini tuzo hizo
zitawafikisha pale ambao wao wamekusudia na vile vile kuibua vipaji
vingine katika tasnia hiyo.
JB
alisema kuwa tuzo hizo zitawafanya mashabiki wao kujua undani wa fani
yao kwa kuwajua watunzi bora, wapiga picha bora na wengineo
No comments:
Post a Comment