Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Chokocho Idrisa Daudi Ame (Kushoto) akipokea
mfuko wa saruji kutoka kwa mkuu wa Kanda ya Zanzibar inayohusiha mikoa
ya Lindi na Mtwara Bw. Hussein Nguvu kama ishara ya kupokea vifaa hivyo.
Kulia ni meneja wa TTCL Pemba Bw. Alphonce Gakwavu.
mfuko wa saruji kutoka kwa mkuu wa Kanda ya Zanzibar inayohusiha mikoa
ya Lindi na Mtwara Bw. Hussein Nguvu kama ishara ya kupokea vifaa hivyo.
Kulia ni meneja wa TTCL Pemba Bw. Alphonce Gakwavu.
Mkuu wa Biashara kanda ya Zanzibar bw. Hussein Nguvu (Kulia)
akimkabidhi sehemu ya Nondo Mwalimu mkuu wa Skuli ya Chokocho Idrisa
Daudi Ame
akimkabidhi sehemu ya Nondo Mwalimu mkuu wa Skuli ya Chokocho Idrisa
Daudi Ame
Mkuu wa Biashara kanda ya Zanzibar Bw. Husssein Nguvu akimkabidhi simu
za mkononi Mkuu wa polisi wa Wilaya Mkoani-Pemba Muhidin Juma Mohamed.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Polisi Jamii Jondeni Sheha M. Sheha
za mkononi Mkuu wa polisi wa Wilaya Mkoani-Pemba Muhidin Juma Mohamed.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Polisi Jamii Jondeni Sheha M. Sheha
Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) imetoa msaada wa vitu mbali mbali
ikiwa ni pamoja na Mifuko ya saruji, nondo pamoja na mchanga katika
skuli ya Chokocho mkoani Pemba.
Akiongea wakati wa kukabidhi msaada huo, Mkuu wa Biashara wa Kanda
ya Zanzibar inayojumuisha mikoa ya Lindi na Mtwara Bw. Hussein Nguvu
amesema, TTCL ina vipaumbele vingi lakini wameamua kuchangia katika
shule kwani wanatambua Elimu ni Mlima, kadri unavyozidi kupanda, ndivyo
unavyozidi kuona mbali.
Naye mwalimu mkuu wa skuli ya Chokocho Bw. Idrisa Daudi Ame amesema,
wanashukuru sana kwa msaada huo kwani utaleta ahueni katika shule hiyo
iliyo na changamoto nyingi ikiwamo uchakavu kwani ilianzishwa miaka
mingi iliyopita.
Wakati huo huo, Mkuu huyo wa kanda ya Zanzibar Bw. Hussein Nguvu amekabidhi
Vifaa mbali mbali ikiwa ni pamoja na simu za mkononi, viatu vya tope
(gum boots) makoti ya mvua (rain coats), vizibao (Reflective jackets)
tochi pamoja na filimbi kwa Polisi Jamii Jondeni mjini Pemba.
Akiongea wakati wa kupokea vifaa hivyo Mkuu wa polisi wa Wilaya Mkoani
Pemba Muhidin Juma Mohamed ameishukuru kampuni ya TTCL kwa kushirikiana
na Jeshi la polisi na hasa Polisi jamii, kwani ulinzi unaenda sambamba
na mawasiliano, hivyo simu hizo na vifaa vingine vitawasaidia sana kiutendaji.
Naye mwenyekiti wa Polisi jamii Jondeni Bw. Sheha M. Shaha amesema,
anaishukuru TTCL kwa msaada huo kwani utawaongezea ufanisi katika utendaji
wa kazi pia amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuwa karibu na jamii na
hasa kiutendaji, na ndio maana wamefanikiwa kufika hapo walipo na wanaweza
kufanya kazi kiufanisi bila shuruti.
No comments:
Post a Comment