Sunday, June 17, 2012

MCHEZA SINEMA MAARUFU TOKA MAREKANI KUKIMBIA MBIO ZA MT. KILI MARATHON

MCHEZA SINEMA MAARUFU TOKA MAREKANI KUKIMBIA MBIO ZA MT. KILI MARATHON

Mcheza sinema maarufu duniani kutoka nchini Marekani Deidre Lorenz atakimbia mbio za kila mwaka za Mount Kilimanjaro Marathon zinazoanza kutimua vumbi kuanzia tarehe 24 Juni mwaka huu kutoka Moshi Club mjini Moshi.


Mbio hizi zilizoanzishwa na mama Marie France kutoka katika mji wa Bethesda, Maryland nchini Marekani mwaka 1991 ni mbio zinazojulikana kama 7 continental Races na zimeshawahi kupata tuzo mbalimbali za kimataifa.

Ujio wa mcheza sinema huyu aliyecheza sinema nyingi kama vile Santorini Blue, Perfect Strangers, The Great Fight, na nyingine nyingi unaiweka Tanzania katika macho ya dunia na kuwavutia watalii wengi kutoka taifa hili tajiri duniani. Deidre Lorenz alizaliwa katika jiji la Oregon nchini Marekani lakini akahamia katika jiji la New York City linalijulikana kama "The Big Apple" nchini Marekani akiwa na kampuni yake ya kutengeneza sinema inayoitwa Thira Films LLS.

Eidre Lorenz ameshawahi kuteuliwa zaidi ya mara tatu kugombe tuzo za wacheza sinema maarufu duniani zinazojulikana kama Grammy Awards. Mcheza sinema huyu ataambatana na Wamarekani wengine kuja nchini tarehe 21 Juni kukimbia mbio hizi ambazo zimetokea kuutangaza sana mji wa Moshi tangu mwaka 1991. Lorenz alipatikana katika bahati nasibu iliyochezwa wakati wa mbio za New York Marathon mwaka jana.

  
Naye mwanzilishi wa mbio hizi mama Marie Frances ana historia ya kuanzisha mbio na matamasha mbalimbali duniani. Alikuwa pia mwanzilishi wa mbio za Pyramid Marathon nchini Misri pamoja na Miss Universe Egypt matamasha yaliyojizolea sifa kemkem.Aliombwa kuja kuanzisha mbio za Marathon nchini Tanzania na balozi wa Tanzania wa wakati ule nchini Misri.Mbio za Mt. Kilimahjaro Marathon ni moja kati ya mbio tafauti za marathon zinazifanyika katika mji wa Moshi.

 Mount Kilimanjaro Marathon zitaanzia Moshi Club mpaka Rau madukani na kurudi mara tatu ambazo zitakuwa kilimeta 42. Kutakuwa pia na mbio z akilometa 21, kilimeta 10 na kilometa 5 kwa watoto. Wakimbiaji hawahitaji kuwa na ujuzi wa kukimbia watu wote wanaweza kukimbia.

No comments:

Post a Comment