DAR ES SALAAM, Tanzania
BONDIA
wa Urusi Vitaly Shemetov ambaye anajulikana Kwa jina la ‘Siberian
Tiger’ ameingia mitini yeye na kocha wake baada ya kupelekewa tiketi za
ndege ya shirika la Kirusi la Aeroflot na kuonyesha kumuofia mpinzani
wake Rashid Matumla wa Tanzania.
Kwa mujibu Rais wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa Afrika(IBF)hii
ni mara ya kwanza kwa mpambano wa kimataifa ulioandaliwa kwa pesa
nyingi kutofanyika baada ya bondia huyo kuingia mitini kwa woga.
Ngowi
alisema Matumla anayejulikana kama Snake Boy ana rekodi ambayo mpaka
sasa hakuna bondia yeyote wa Kitanzania aliyeweza kuifikia.“Matumla ameshawahi kuwa bingwa wa Taifa, Afrika Mashariki na Kati, Bara la Afrika, Mabara na Dunia aliyetambuliwa na Umoja wa Ngumi Duniani (WBU)alisema Ngowi na kuongeza akiwa chini ja DJB Promotions bondia Rashid Matumla ambaye kwa sasa ndiye Kamishna wa TPBC kanda maalum ya Dar-Es-Salaam alionyesha ubingwa wa hali ya juu.
Alisema Matumla amepangiwa kupigana na bondia mwingine siku za usoni ili kupooza machungu ya kukimbiwa na Mrusi huyo.
“Mrusi
wa Matumla amemkimbia baada ya kuona rekodi yake ni kali, wawili hao
walikuwa wacheze katika mpambano uliopewa jina la ‘The Rumble on the
Mountain’ na ulikuwa ushuhudiwe na mcheza sinema maarufu kutoka nchini
Marekani Deidre Lorenz ambaye atakuwa anashiriki mbio za Mount
Kilimanjaro marathon mjini Moshi Juni 24 mwaka huu”alisema Ngowi.
No comments:
Post a Comment