Sunday, June 17, 2012

MWANAUME ALIYEOTA MATITI!!!


BAGAMOYO
Mkazi wa kijiji cha Magomeni Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani,  Khamisi Tanga (46), ameota  matiti katika hali isiyo ya kawaida ikidaiwa imesababishwa na kutumia dawa za kupunguza  makali ya Ukimwi   ARV’S.
     Akizungumza na waandishi wa habari waliokwenda Wilayani humo kufanya utafiti kuhusu utekelezaji wa sheria ya Ukimwi na Chama cha Waandishi wa habari za Ukimwi (AJAT),Khamisi (Pichani) alisema alipatwa na mkasa huo miaka mitatu iliyopita.
    Akisimulia namna alivyoanza kuugua alisema awali aliona matiti yake yakiongezeka ukubwa kila kukicha lakini hakujua kama lingeweza kuja kuwa tatizo kubwa kama lilivyo sasa.
    Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya ilimbidi kwenda kliniki anayohudhuriaga kupata dawa na kuwaeleza manesi ambapo walimjibu kuwa imesababishwa na dawa anazotumia na hivyo kulazimika kukatizwa dozi hiyo na kupewa aina nyingine.
    Hata hivyo Khamisi alisema kwamba pamoja na kubadilishiwa dozi hajaona kama kuna mabadiliko yoyote aliyoyapata na kuongeza kwamba hivi karibuni alipewa dawa nyingine ambazo kati ya hizo kuna zile ambazo zilimsabishia matiti na tayari ameanza kupatwa na maamuvu aliyokuwa akisikiaga awali wakati matiti yalivyokuwa yanaanza kuota.
     Kwa mujibu wa Khamisi ameshahangaika kupata matibabu hadi Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili lakini hadi leo hajapatiwa tiba stahili ya kumaliza tatizo hilo.
    “Jamani Watanzania naomba wanisaidie kwa njia yoyote ile ili niondekane na hali hii kwani inanidhoofisha sana na kunikosesha raha hasa mbele ya wanaume wenzangu.
Kwani hapa navyoongea na nyie waandishi nilipimwa hadi kansa na matiti ndio kama hivyo mnavyoyaona yanaendelea kukua na huniuma sana hasa wakati ninapolala,”alisema kaka huyo.
Pia alitumia fursa hiyo kumuomba Rais Jakaya Kikwete kumsaidia ili arudi katika hali yake ya uanaume kwa kuwa maisha kwa sasa kwake yamezidi kuwa magumu kwa kuwa hawezi kufanya kazi yoyote kutokana na hali hiyo.
Kwa upande wa mtaalam wa magonjwa, Dk. Dina Komakoma,akielezea kuhusu sababu za kutokewa kwa hali hiyo kwa wagonjwa wenye maambukizi ya VVU ni jambo la kawaida japo hutofautiana.
Dk. Komakoma alisema wengine hujikuta wakinenepa au wakikonda sana na hili la Khamis sio mtu wa kwanza kupatwa na hali hiyo na kuongeza kwamba inapotokea mgonjwa akapata hali tofauti kama hiyo anapaswa kusitishiwa dawa. SOURCE MITANDAO

No comments:

Post a Comment