Thursday, June 28, 2012

SAFARI LAGER YATANGAZA KUDHAMINI MASHINDANO YA TANZANIA INTERNATIONALOPEN DARTS CHAMPIONSHIPS JIJINI MWANZA.


  Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu udhamini wa mashindano ya Darts yanayojulikana kwa “Tanzania International Open Darts Championships” yanayotarajiwa kuanza kesho jijini Mwanza.Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Darts Taifa, Gesase Waigama.

  Mwenyekiti wa Chama cha Darts Taifa, Gesase Waigama (kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu udhamini wa Safari Lager kwenye mashindano ya Darts yanayojulikana kwa “Tanzania International Open Darts Championships” yanayotarajiwa kuanza kesho jijini Mwanza.Kulia ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza rasmi kudhamini mashindano ya Kimataifa ya mchezo wa Darts yatakayojulikana kwa “Tanzania International Open Darts Championships” ambayo yanatarajiwa kuanza rasmi kesho Ijumaa Julai 01,2012 jijini Mwanza .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, meneja wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo amesema Safari Lager imesaidia kiasi cha MILIONI 32 za kuendesha mashindano hayo ikiwa ni pamoja na zawadi za vikombe na pesa taslimu.“Safari Lager inaendeleza lengo lake la kusaidia kukuza zaidi mchezo wa Darts hapa Tanzania.Alisema Bw. Shelukindo. Safari Lager imekuwa ikidhamini mashindano mbalimbali ya mchezo wa Darts, na imegawa pia vifaa vya michezo kwa maeneo mbalimbali ya kuchezea Darts Dar Es Salaam na mikoani.
Naye mwenyekiti wa Taifa wa chama cha Darts cha Taifa (TADA) Bw. Gesase N. Waigama, ambaye pia ni raisi wa shirikisho la Darts Afrika Mashariki alisema timu shiriki katika mashindano haya ni Kenya,Uganda,Tanzania na Rwanda.
Gesase alisema mtindo utakaotumika katika mchezo huo ni wa Kitaifa kwa kushirikisha timu ya taifa ya kila nchi,Vilabu,Doudles na Singles.
Mashindano hayo yataanza kesho katika Hotel ya Monac Kirumba na yanatarajiwa kufikia tamati jumapili Julai 3,2012 jijini Mwanza

1 comment: