Mwenyekiti wa Chama cha Darts Taifa, Gesase Waigama (kulia)
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu udhamini wa Safari Lager kwenye
mashindano ya Darts yanayojulikana kwa “Tanzania International Open Darts
Championships” yanayotarajiwa kuanza kesho jijini Mwanza.Kulia ni Meneja wa Bia
ya Safari Lager, Oscar Shelukindo
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia
yake ya Safari Lager leo imetangaza rasmi kudhamini mashindano ya
Kimataifa ya mchezo wa Darts yatakayojulikana kwa “Tanzania
International Open Darts Championships” ambayo yanatarajiwa kuanza rasmi kesho
Ijumaa Julai 01,2012 jijini Mwanza .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, meneja wa
bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo amesema Safari Lager imesaidia kiasi
cha MILIONI 32 za kuendesha mashindano hayo ikiwa ni pamoja na zawadi za vikombe
na pesa taslimu.“Safari Lager inaendeleza lengo lake la kusaidia kukuza zaidi
mchezo wa Darts hapa Tanzania.Alisema Bw. Shelukindo. Safari Lager imekuwa
ikidhamini mashindano mbalimbali ya mchezo wa Darts, na imegawa pia vifaa vya
michezo kwa maeneo mbalimbali ya kuchezea Darts Dar Es Salaam na
mikoani.
Naye mwenyekiti wa Taifa wa chama cha Darts cha Taifa (TADA) Bw. Gesase
N. Waigama, ambaye pia ni raisi wa shirikisho la Darts Afrika Mashariki alisema
timu shiriki katika mashindano haya ni Kenya,Uganda,Tanzania na Rwanda.
Gesase alisema mtindo utakaotumika katika mchezo huo ni wa Kitaifa kwa
kushirikisha timu ya taifa ya kila nchi,Vilabu,Doudles na Singles.
adidas tubular
ReplyDeletecheap jordans
louboutin outlet
nike air max 270
michael kors bags
nike 97
adidas superstars
coach factory outlet
golden goose
golden goose sneakers