MCHEZA
sinema maarufu kutoka Marekani, Deidre Lorenz, jana amezipamba mbio za
Mt. Kilimanjaro Marathon zilizotimua vumbi kuanzia saa mbili asubuhi
kutoka klabu maarufu ya Moshi hadi Rau madukani.
Lorenz
alikuwa mmoja wa wakimbiaji zaidi ya 200 kutoka katika nchi za
Marekani, Canada, Uingereza, India, Australia, Brazil na Tanzania.
Kushiriki
kwa mcheza sinema huyo maarufu wa sinema za Santorini Blue (ambayo
ilitegenezwa kwenye fukwe za mahaba za kisiwa cha Santorini nchini
Ugiriki), Perfect Strangers, The Big Fight na nyingije nyingi imezifanya
mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon kuwa na hadhi ya kipekee katika mbio
za marathon hapa Afrika.
Mbio
hizi zilizoanzishwa na Marie Frances kutoka katika jiji la matajiri la
Bethesda nje kidogo ya jiji la Maryland kule Marekani zimetimiza miaka
22 toka zianzishwe mwaka 1991. Mt. Kilimanjaro Marathon zilizishwa baada
ya balozi wa zamani wa Tanzania nchini Misri kumwomba Marie Frances
kuja Tanzania na kuanzisha mbio zenye hadhi ya kimataifa. Mt.
Kilimanjaro Marahon zimeshawahi kushinda tuzo mbalimbaliza kimataifa
zilizotolewa na Wonders of the World Magazine ambalo lina wasomaji zaidi
ya miloioni 5 na kuzipa nafasi ya pili na wakati gazeti maarufu duniani
la Forbes lilizipa nafasi ya kwanza kati ya mbio zinazojulikana kama
Seven Continental Races.
Kutokana
na kuutangaza mji wa Moshi kwa kiwango kikubwa kimataifa Manispaa ya
Moshi ilimpa barabara inayojulikana kama Marie Frances Boulevard pamoja
na funguo za Manispaa ya Moshi na Cheti ya ukazi wa kudumu.
Mkimbiaji
kutoka jiji la Arusha Getuni Tsekewey aliibuka kidedea wa mbio za
kilometa 42 kwa kukimbia kwa saa 2 na dakika 26 nukta 30 wakati
Nicodemus Hiiti kutoka Kilimanjaro alikuwa wa 2 kwa kukimbia saa 2 na
dakika 38 nukta 20 naye Shauri Habiye kutoka Arusha alikuwa wa tatu kwa
kukimbia saa 2 na dakika 38 nukta 24.
Wengine
ni Samwel Lucian kutoka Kilimanjaro aliyenyakua nafasi ya 4 kwa
kukimbia kwa saa 2 dakika 38 nukta 47 wakati Petro Gimanya wa
Kilimanjaro alitimka kwa saa 2 dakika 57 nukta 18 na kushika nafasi ya
5.
Katika
mbio za Marathon upande wa wanawake Banuelia Brighton alitimua vumbi na
kushika nafasi ya kwanza kwa saa 3 dakika 06 nukta 01 wakati Flora Yada
alimfuatia kwa mbali kwa kukimbia kwa saa 3 dakika 38 nukta 08.
Kwa
upande wa mbio za nusu marathon wanariadha kutoka Arusha walinyakua
nafasi zote. Peter Sule alikimbia kwa saa 1 dakika 07 nukta 42 na kuwa
wa kwanza, Mohamed Duley alishika namba mbili kwa kikimbia kwa saa 1
dakika 07 sekunde 98 wakati Said Hassan alitimka kwa saa 1 dakika 10
sekunde 25 na kuwa wa tatu.
Nusu marathon kwa wanawake kulikuwa na mkimbiaji mmoja tu ambapo Farida Guse wa Arusha alikimbia kwa saa 3 dakika 22 sekunde 22.
Mbio
za kilometa 10 (10K) ziliwashirikisha wageni tu ambapo kwa upande wa
wanaume Sander Markos kutoka Marekani alishika nafasi ya kwanza kwa
kukimbia kwa saa 1 dakika 01 sekunde 20 na Malcom Frazer pia kutoka
Marekani alikimbia kwa saa 1 dakika 20 sekunde 22 na kuwa wa pili.
Kwa
upande wa wanawake mbio za kilometa 10 (10K) kwa wageni Cindy Johanson
kutoka Kanada alikuwa wa kwanza kwa kukimbia kwa saa 1 dakika 12 sekunde
22, Marika Johson alishika nafasi ya pili kwa kukimbia kwa saa 1 dakika
20 sekunde 48, Talia Peter kutoka Marekani alikuwa wa tatu kwa kukimbia
kwa saa 1 dakika 26 sekunde 04.
Naye
mcheza sinema maarufu kutoka Marekani Deidre Lorenz alimaliza mbio za
kilomita 42 na kufanya kuwa mbio za tatu za marathon alizowahi kukimbia
baada ya zile za New York Marathon mwaka 2010 na 2011.
Lorenz
aliondoka na ndege ya shirika la Ethiopia Airlines kurudi kwake "The
Big Apple" kama linavyojulikana jiji la New York la Marekani ambapo
hufanya shughuli zake za kucheza sinema.
No comments:
Post a Comment