Salum Suleiman 'Sule Junior'
Mwandishi Wetu
Bonanza
kubwa la mchezo wa mpira wa miguu linaloitwa 'Nane nane soccer bonanza'
linatarajiwa kufanyika kwenye viwanja vya Tanganyika Parkers Kawe
jijini Dar es Salaam siku ya kilele cha sherehe za nane nane.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa kampuni ya SULE'S INC. &
ENTERTAINMENT, Salum Suleiman ambao ndiyo wadhamini wa Bonanza hilo timu
mbalimbali kutoka katika maeneo ya wilaya ya Kinondoni jijini Dar es
Salaam zitashiriki.
"Maandalizi
ya bonanza hili yameshafikia katika hatua nzuri kabisa, Kamati imefanya
kazi nzuri mpaka kufikia hapa na tunategemea bonanza hili litafanyika
kwa mafanikio makubwa,"alisema Suleiman.
Akizungumzia
timu zitakazoshiriki katika bonanza hilo, Suleiman alisema,"tunatarajia
kuwa na timu nane ambazo zitachuana katika kuwania kombe siku hiyo na
mashindano yataendeshwa kwa mtindo wa mtoano."
Alisema
wameamua kuliendesha bonanza hilo kwa mtindo wa mtoano ili timu ziweze
kutoa ushindani wa kutosha na kuburudisha watu watakaojitokeza katika
bonanza hilo.
"Washindi
watapata zawadi, kwa sababu mshindi wa kwanza atatwaa kombe, mshindi wa
pili pia atapata zawadi, mchezaji bora, mfungaji bora, kipa bora na
mchezaji mwenye nidhamu wote hao watapata zawadi."
Sherehe za nane hufanyika kila mwaka sehemu mbalimbali nchini ikiwa ni siku ya kuadhimisha siku ya wakulima.
No comments:
Post a Comment