Moja ya
gari maalum kwa ajili ya kufagia barabara (Road sweeper) gari hilo linafagia
barabara na kumwaga uchafu mbali zaidi.maonyesho hayo yamefanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo.
Mkuu wa
mkoa wa Dar es Salaam Mhe, Said Meck Sadick akizungumza na waandishi wa habari
kuhusiana na Operesheni ya usafi inayoendelea katika Manispaa ya Ilala ambapo
aliwataka wananchi wa ilala kuwa na Ushirikiano kwa kutoegesha magari ovyo
pasipo utaritibu ili waweze kupisha magari ya kufanyia usafi.
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
Rachel Charles
MKURUGENZI Mtendaji wa Ear promotion Bw.Brian Kikoti amewaomba wafanyabishara ndogondogo wa soko la wamachinga complex kupeleka bidhaa zao na sio kuliacha mpaka lichangamke.
Ameyasema hayo leo alipokuwa anaongea na wafanyabiashara katika
soko la wamachinga jijini Dar es salaam, alisema wafanyabiashara
ndogondogo hawapaswi kulikimbia soko hilo kwa madai kuwa hakuna wateja.
Bw.Kikoti alisema wamachinga wote wanapaswa kushirikiana na ear
promotion ili kulitangaza soko hilo ndani na nje ya nchi ili kukuza
uchumi kwa wafanyabiashara waweze kujikimu kimaisha na ata kukuza uchumi
wa Taifa.
Pia alisema ili kulifanya soko hilo litambulike kimataifa watakuwa
na maonyesho ya gulio litakalofanyika kila mwaka mwezi wa tisa kwa muda
wa siku 14 ili kuwasaidia wafanyabiashara hao kutangaza bidhaa zao kwa
uraisi.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Ear Promotion Bw. Frank Miti alisema
kila sikukuu wataleta makampuni mbalimbali ili kuunga mkono mawazo na
kuwawezesha wafanyabiashara hao kupata faida kubwa.
Aidha Wafanyabiashara ndogondogo wamelipongeza jambo hilo kwa kuwa
litawapa fursa ya kuingia kwenye ushindani na kubadilishana biashara
na Nchi nyingine hivyo kupata misaada kutoka kwa wafadhili.
No comments:
Post a Comment