Mabondia Thomas Mashali na Maisha Samson wamemaliza zoezi zima la upimaji na tayari kwa ajili ya mpambano wao utakao fanyika katika ukumbi wa Friends corner hotel-manzese siku ya jumapili 24/6/2012. mpambano huo wa ubingwa wa taifa wa TPBO uzito wa midle na unaosimamiwa na TPBO chini ya rais wake Yasin Abdallah na katibu mkuu Ibrahim Kamwe umemalizika vizuri na mabondia wote wapo katika hali nzuri na tayari kwa fight.
pia kutakuwa na mapambano ya utangulizi kama ifuatavyo;
juma fundi(52kg) v/s shaban madilu (49.5kg) - watacheza raundi nane mohamed shaban'ndonga' (61kg) vs Musa hassan (61kgs) - watacheza raundi sita Jonas godfrey (61.5kgs) vs Venance mponji(59kg) - watacheza raundi sita Abdalah mohamed'prince naseem'(64kgs) vs Yohana Mathayo(65.5kgs)- raundi sita Nasoro Hatibu 55kg vs Abdul Athuman 55kgs -watacheza raundi nne
Martin Richard 50kgs vs Hassan Kadenge 49kgs -watacheza raundi nne
ngumi zitaanza kama kawaida kuanzia saa kumi jioni, na tunarudia tena kusema katika ngumi hakuna kupendelea na TPBO itasimamia kwa haki zote bila kuangalia mtu. tutakachoangalia ni mchezo kuchezwa kwa kanuni za ngumi na utoaji points kulingana na bondia anavyoscore kwa ngumi halali sio kulingana na makelele ya washabiki
Katika Mchezo huo kutakua na DVD Mpya kabisa za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja
na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha
wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa
ajili
ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua
sheria za masumbwi.Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny
Paquaio, Amiri
Khani,
Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na
matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa
dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa
No comments:
Post a Comment