Mashali akivalishwa mkanda wake wa ubingwa baada ya kuutetea jana kwa kumtwanga TKO raundi ya tano Maisha |
Na Prince Akbar
BAADA ya kumtwanga kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya tano Samson Maisha wa Mbeya, bingwa wa Taifa wa TPBO, Thomas Mashali 'Simba wa Teranga' amesema anamtaka mshindi wa pambano kati ya Japhet Kaseba na Francis Cheka apande naye ulingoni, ili adhihirishe yeye ndiye ‘king’ wa ndondi Tanzania.

Mashali akiwa amemdondosha Maisha jana |
Akizungumza na BIN ZUBEIRY kwenye ukumbi wa Friends
Corner, Manzese jana baada ya ushindi wake huo, Mashali alisema kwamba anaamini
kwa sasa katika nchi hii hana mpinzani na ameomba yeyote atakayeshinda kati ya
Kaseba na Cheka asikwepe kupanda naye ulingoni.
“Huyu mtoto (Maisha), si saizi yangu, wamempakazia tu, baada
ya kuona mabondia wote wa Dar es Salaam sasa hivi wananiogopa, nilikuwa nampiga
huku namhurumia, na bado amefia katikati ya safari (raundi ya tano). Namtaka mshindi
kati ya Kaseba na Cheka,”alisema Mashali.
Katika pambano hilo la jana la uzito wa Middle, Mashali alimzidi
uwezo mpinzani wake kuanzia raundi ya kwanza na katika raundi ya tano
alimkalisha chini kwa ngumi kali ya mkono wa kulia.
Maisha alijitutumua kuinuka ili aendelee na pambano, lakini
alionekana dhahiri hajiwezi na ndipo Kocha wake, Bagaza Mambane akarusha taulo
ulingoni. Hata hivyo, Maisha anaonekana ni bondia mzuri akipata mazoezi zaidi
na ujanja wa katika masumbwi.
No comments:
Post a Comment