WAANDISHI wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wamekutana
jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuunda Mtandao utakaoweza kusimamia,
kupigania pamoja na kutetea haki zao.
Akizungumza katika kikao hicho juzi Katibu wa muda aliyeteuliwa
na waandishi hao, Ebeneza Mende alisema kuwa mtandao huo utajulikana kwa jina la
‘Waandishi wa Habari Tanzania ‘ (TAJONET).
Alichanganua kuwa
mtandao huo hutatumika kama chachu ya kusaidiana katika matatizo mbalimbali,
ukiwa na sauti moja katika kutetea maslahi yao, huku ukihusika moja kwa moja katika kusimamia maadili ya tasnia
ya habari ambayo yanadaiwa kuporomoka.
Mende alisema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya wandishi wa
habari kujikuta wakikabiliwa na matatizo mbalimbali huku wakikosa msaada.
Aidha, alibainisha kuwa TAJONET utakuwa bega kwa bega katika
kuangalia suala zima la afya ya wananchama kwa kuangazia ngazi ya chini kama
matibabu awapo hospitalini, pamoja na msiba.
“Watu wengi wamekuwa wakichukulia matatizo ni kifo, bila kuangalia
mambo mengine kama ugonjwa, sisi hatutaki kujielekeza hivyo bali tunataka
ltatizo la ugonjwa lipewe
kipaumbele ili kuepusha
vifo visivyo na ulazima”alisema Mende.
No comments:
Post a Comment