■Ataitangaza Tanzania na vivutio vyaka
kwa wacheza sinema na walimbwende wengine wa
Marekani.
Mcheza sinema maarufu na mlimbwende
Deidre Lorenz kutoka katika jiji la New York nchini Marekani ameteuliwa kuwa
balozi wa Mt. Kilimanjaro Marathon kwenye jiji hili la mapesa duniani la New
York City (NYC).
Uteuzi huo ulifanywa kwa pamoja kati
ya Rais wa Mt. Kilimanjaro Marathon 1991 Mtanzania Onesmo Ngowi na mwanzilishi
wa mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon Mmarekani Marie Frances hivi karibuni.
Uteuzi wa Lorenz ulizingatia uwezo
wake wa kujichanganya katika makundi mbalimbali nchini Marekani hususan kundi
la vijana matajiri. Hawa ndio wanaoweza kuwa watalii wenye uwezo wa kulipa pesa
nyingi kwa huduma wanazopata watembeleapo vivutio mbalimbali vya kitalii nchini
Tanzania.
Aidha, Lorenz anao uwezo wa
kuunganisha wacheza sinema na walimbwene wengine na kuwashawishi kuja
kutembelea vivutio mbalimbali hapa Tanzania.
Deidre Lorenz alizaliwa katika jiji
la Oregon na alianza kijihushisha na uchezaji wa vipindi watoto vya televisheni
kabla ya kuhamia kwenye jiji la New York ambako alijiingiza kucheza filamu.
DeidreLorenz
ameshacheza sinema nyingi kati ayke zikiwa zifuatazo: Santorini Blue, The Great
Fight, Perfect Strangers na kuwahi kupata tuzo za: Tuzo ya Produza
mpayailiyotolewa na Downtown Boca FilmFestival 2011 na kukabidhiwa na
Stella Artois, tuzo ya chaguo la wadau wa sinema iliyotolewa na The NYC
Downtown, tuzo ya TorontoIndependent iliyotolewa na Film Festival 2010. Mbali
ya tuzo hizo Lorenz amewahi kupata tuzo mbalimbali za Oscar kama muingizaji
bora.
Akitumia kampuni yake ya Thira Films
LLC, Lorenz amekuwa anauza sinema zake kwenye miatandao mbalimbali. Hivi
karubuni aliingia mkataba na kampuni ya Google kuuza kazi zake kwenye mtandao
huu mkubwa duniani.
Kuteuliwa kwa Lorenz kunaipa Tanzania
nafasi ya kujitangaza zaidi kwa kutumia mcheza sinema huyu maarufu duniani na
hivyo kuipa nafasi kubwa nchi hii kujulikana zaidi kwa wacheza sinema ambao
hupenda kutembelea maeneo ya kitalii.
No comments:
Post a Comment