Na.Ashura Mohamed-Arusha
Halamshauri ya manispaa ya Arusha imesema kuwa kuanzia sasa itaanza rasmi kutenga bajeti kwa ajili ya kuwasaidia yatima ndani ya manispaa , ambapo bajeti hiyo pia italenga misaada kwa vituo mbalimbali ili kupunguza changamoto mbalimbali ambazo zinaikabili vituo mbaliombali hapa mjini
Akizungumza katika harambee kwa ajili ya watoto yatima wa kituo cha watoto Matonyok Children Care kilichopo katika kata ya Olasistri Meya wa jiji la Arusha Bw Gaudence Lyimo alisema kuwa mpango huo utaanza hivi karibuni ambapo vituo vya mayatima navyo vitahusika kwa kuwa kwa sasa kuna changamoto mbalimbali ambazo zinakabili vituo vya yatima.
Bw Lyimo alisema kuwa kwa sasa bajeti hityo itahakikisha kuwa hata misada mbalimbali ambayo inatolewa na wafadhili mbalimbli inawafikia walengwa ambapo yote hayo yatakuwepo ndani ya bajeti hiyo.
“kwa sasa tumepanga kuwa katika kila bajeti ya halmashauri yatima nayo wanatakiwa kuhusishwa kwa kuwa ndani ya vityuo vingi vya mayatoma kuna changamoto ambazo zinafanya baadhi ya mayatima kushindwa kufikia malengo yao”alisema Bw Lyimo
Pia aliongeza kuwa mpango huo wa kuwapa yatima ufadhili mbalimbali kupitia halmashauri hiyo pia wataweka mpango maalumu wa kuhakikisha kuwa wanawafuatilia baadhi ya vituo ambavyo vinatumia vibaya ufadhili pamoja na jina la yatima.
Hata hivyo harambee hiyo ambayo iliandaliwa na diwani wa kata hiyo Bi Rehema Mohamed yatima walifanikiwa kupata million mbili , na laki moja ambapo fedha hizo zitatumika kwa matumizi mbalimbali ya Yatima hao
Bi Rehema alieleza kuwa ni vema kama kila jamii ihakikishe kuwa inawalinda na kuwathamani mayatima na badala yake kuwapa haki zao za msingi kwa kuwa kwa sasa ndani ya vituo vingi kuna changamoto ikiwemo suala zima la ukame
Alimalizia kwa kusema kuwa kutokana na changamoto ambazo zimo kwenye vituo wengi wa mayatima wanakosa haki zao za msingi jambo ambalo linawafanya waweze kukimbia katika vituo vyao ambavyo wanalelewa.
No comments:
Post a Comment