Meneja
Uhusinao wa Airtel, Jackson Mbando, akizungumza katika uzinduzi wa
promotion kabambe kwa wateja wao ijulikanayo kama “kula Dabo” kupitia
huduma ya Airtel Money. Uzinduzi wa promotion hiyo ameufanya leo katika
viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam(DITF)
maarufu Saba Saba yanayopendelea katika barabara ya Kilwa jijini.
Meneja
Uhusinao wa Airtel, Jackson Mbando,(aliye chuchuma mbele) akipiga picha
ya pamoja na baadhi ya vijana wanaotoa huduma mbalimbali katika banda
la Airtel, baada ya uzinduzi wa promotion kabambe kwa wateja wao
ijulikanayo kama “kula Dabo” kupitia
huduma ya Airtel Money. Uzinduzi wa promotion hiyo ameufanya leo katika
viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam(DITF)
maarufu Saba Saba yanayopendelea katika barabara ya Kilwa jijini. .
Meneja
Uhusinao wa Airtel, Jackson Mbando, akizungumza katika uzinduzi wa
promotion kabambe kwa wateja wao ijulikanayo kama “kula Dabo” pia
alimpigia simu mteja mmoja mara baada ya kuibuka mshindi wa zawadi za
papo kwa papo ndani ya saba saba. Uzinduzi wa promotion hiyo ameufanya
leo katika viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es
Salaam(DITF) maarufu Saba Saba yanayopendelea katika barabara ya Kilwa
jijini. Kulia ni Ofisa wa Airtel Money, Bahati Straton
Afisa wa Airtel 3G, Teher Abdulrahman, akichagua kikaratasi cha mshindi katika Bahati
nasibu ya Papo kwa Papo katika viwanja vya sabasaba ndani ya Kijiji cha
Airtel. Kushoto ni Meneja Uhusinao wa Airtel, Jackson Mbando na
Katikati ni Ofisa wa Airtel Money, Bahati Straton, Airtel pia ilizindua
promotion ya “Kula Dabo” kwa wateja wao watakao nunua bidhaa kwa Airtel
Money.
KAMPUNI
ya simu za mkono ya Airtel Tanzania jana imezindua promosheni kwa
wateja inayojulikana kama “Kula Dabo” katika maonyesho ya 36 ya biashara
kwenye viwanja vya Sabasaba Temeke.
Akizindua
promosheni hiyo Meneja Uhusiano wa kampuni ya Airtel, Jackson Mmbando
alisema kuwa katika kuhakikisha huduma ya pesa mkononi inamfikia kila
Mtanzania na kupunguza changamoto mbalimbali za kifedha.
Alisema
kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel imeamua kuwazawadia wateja wake
wote wanaonunua salio kupitia simu za mknoni kupata mara mbili ya salio
lolote atakaloongeza kupitia Airtel Money na ataweza kupiga simu na
kutuma sms kwenda mtandao wowote
Promosheni
hii itaendelea katika msimu huu wa sabaSaba ambapo itadumu kwa muda wa
wiki mbili kuanzia sasa, Mmbando alisema “ Airtel kwa kuonyesha
tunawajali wakala wetu wote, mwezi huu kila wakala atapata mara mbili ya
kamisheni yake, lengo letu ni kuhakikisha kila mdau wetu anafaidika na
huduma yetu hii ya Airtel money”
“Wakala
wetu sasa mnakila sababu ya kuhakikisha mwezi huu unafanya mhamala
mingi ili tu muweze kupata kamisheni nyingi kwa kula dabo yako”
aliendelea kusema Mmbando
Vilevile
mbali na kuwepo kwa promosheni ya kula dabo wateja wa Airtel
watakaonunua bidhaa mbali mbali katika viwanja na banda lete la sabasaba
kupitia huduma yetu ya Airtel money wataweza kujishindia zawadi mbali
mbali ikiwemo pesa taslim kuanzia shilingi 2,000, simu za mkononi aina
ya Samsung 1085 pamoja na modem ya 3.75G kupitia droo ya kuchanganya
kuponi itakayofanyika katika viwanja hivyo kila siku saa nane kamili.
Airtel
tunawakaribisha wateja wetu kutembea kijiji cha Airtel katika Maonyesho
ya 36 ya biashara ambayo yataendelea kwa muda wa siku kumi ili
kujipatia huduma zetu mbali mbali ikiwemo ya Airtel Money, kuwezesha
simu yako kutumia intaneti yenye spidi, kujipatia modem za 3.75G kwa
gharama nafuu zaidi pamoja na kujua huduma nyingine nyingi kutoka
Airtel.
Airtel
hivi karibuni ilizindua na kuboresha huduma ya Airtel Money pesa
mkononi na mpaka sasa watanzania wengi wamenufaika kwani imeweza kutoa
ajira kwa watanzania wengi kwa kupitia uwakala hivyo wananchi wengi
wameweza kujipatia mapato kwa kupitia huduma hii, kwa wateja wetu wote
Airtel money ina mawakala zaidi ya 10,000 waliosambaa nchi nzima na
kupitia huduma ya Airtel Money unaweza kutuma na kupokea pesa kutoka
mtandao wowote nchini na utaweza kutuma kuanzia shilingi 1,000 hadi
kiwango cha shilingi 1,000,000 kwa Airtel money.
Maonyesho
ya kimataifa ya Dar es salaam Maarufu kama sabasaba, Ni maonesho ya
kibiashara yanayoongoza Tanzania maonyesho hayo yanayofanyika kwa siku
kumi huvutia wageni zaidi ya milioni nne na kujenga mahusiano na
maingiliano baina ya watoa huduma na wateja wao na kutoa fursa kwa
wateja kuangalia na kulinganisha ubora wa bidhaa.
x
No comments:
Post a Comment