Thursday, July 26, 2012

MWAFAKA WA WALIMU NA SERIKALI WASHINDIKANA


  Rais wa chama cha walimu Tanzania (CWT) Bwana Gration Mukoba
akifafanua kuhusu mgogoro wao baada ya  kushindikana kusuluhishwa na msuluhuishi
aliyeteuliwa na tume ya Usuluhishi na uamuzi juu ya mgogoro wake na
serikali juu  katika madai yao uliotangazwa tarehe 8 / 6 / 2012,  mbele ya
waandishi wa habari jijini Dar es salaam.kushoto ni Mweka hazina wa
chama cha walimu Tanzania bwana Mohamed  Utaly
Rais wa chama Cha walimu Tanzania Bwana Gratian Mukoba akiwaonyesha
waandishi wa habari ( hawapo pichani) Cheti kilichotolewa na Msuluhishi
aliyeteuliwa na tume ya usuluhishi na Uhamuzi kushindikana na kusainiwa
na msuluhishi ndugu Cosmas Fimbo baada ya kujadiliana kwa muda wa siku
30 kama sheria inavyoelekeza.

Ambapo kwa mujibu wa sheria kifungu cha 80-(1) cha sheria ya ajira na

mahusiano kazini ya mwaka 2004,  Chama cha walimu tTnzania kimetoa
wito kwa wanachama wake kuanzia jana tarehe 25/ 6/ 2012 kuanza kupiga
kura ya NDIO au HAPANA kwa wanachama wake wote nchini ili kukubali
kugoma au kusiwepo na mgomo
PICHA NA PHILEMON SOLOMON.  
Baadhi ya waandishi wa habari walioudhulia mkutano huo katika ofisi ya
 chama cha walimu tanzania makao makuu jijini Dar es salaam, wakimsikiliza
 kwa makini Rais wa chama cha walimu (hayupo pichani) hakitoa tamko juu
ya mgogoro huo na serikali baada kushindwa kufikia makubaliano kati yao.

No comments:

Post a Comment