Friday, July 13, 2012

RC TANGA APIGA MARUFUKU UVUNAJI MAZAO YA MISITU



Na Mohammed Mhina, Handeni


MKUU wa Mkoa wa Tanga Bi. Chiku Galawa, amepiga marufuku shughuli zote za uvunaji wa mazao ya misitu katika wilaya ya Handeni na kuunda tume ya kuchunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na vitendo vya ukataji wa miti ya mbao na mkaa.
Mkuu huyo wa mkoa amechukua uwamuzi huo baada ya kushuhudia uharibifu mkubwa wa misitu ambapo aliwakamata watu wawili kwa uhalibifu hao uliokuwa ukifanyika kwa kisingizio cha kuanzisha mashama mapya.
Bi. Galawa amesema kuwa tume hiyo itawashirikisha watumishi wa Idara ya Maliasi na miisitu, Jeshi la Polisi pamoja na watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya handeni.
Amesema kwa vile baadhi ya watu wanaokamatwa katika maeneo ya misitu wamekuwa wakidai kuwa wana vibali vya uvunaji wa mazao ya misitu, kwa hiyo timu hiyo itachunguza uhalali wa vili hivyo na mtoaji.
Bi Galawa amesema amefikia uamuzi huo baada ya kushukudia uharibifu mkubwa wa mazingira katika wilaya ya Handeni na kuwakamata watuhumiwa wawili waliokuwa kwenye msitu wa Kang’ata wilayani humo wakiendelea na ukataji miti ya uwoto wa asili.
“Tume hiyo itachunguza nani ana kibali, kimetolewa na nani na cha muda gani”. Amesema Bi Galawa na kuongeza kuwa kimsingi serikali haiwezi kukaa kimya huku ikiona kuna baadhi ya wananchi wanaoharibu misitu na kuongeza upotevu wa mvua.
Watuhumiwa waliokamatwa na mkuu huyo wa mkoa kwa uharibifu wa misitu ni Abraham Yameti(50) na Augostine Jacob(42) wote wakazi wa Kang’ata wilayani humo.

No comments:

Post a Comment