Na Mohammed Mhina, Handeni
MKUU wa Mkoa wa Tanga Bi. Chiku Galawa, amepiga marufuku shughuli zote za uvunaji wa mazao ya misitu katika wilaya ya Handeni na kuunda tume ya kuchunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na vitendo vya ukataji wa miti ya mbao na mkaa.
MKUU wa Mkoa wa Tanga Bi. Chiku Galawa, amepiga marufuku shughuli zote za uvunaji wa mazao ya misitu katika wilaya ya Handeni na kuunda tume ya kuchunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na vitendo vya ukataji wa miti ya mbao na mkaa.
Mkuu
huyo wa mkoa amechukua uwamuzi huo baada ya kushuhudia uharibifu mkubwa
wa misitu ambapo aliwakamata watu wawili kwa uhalibifu hao uliokuwa
ukifanyika kwa kisingizio cha kuanzisha mashama mapya.
Bi.
Galawa amesema kuwa tume hiyo itawashirikisha watumishi wa Idara ya
Maliasi na miisitu, Jeshi la Polisi pamoja na watumishi wa halmashauri
ya Wilaya ya handeni.
Amesema
kwa vile baadhi ya watu wanaokamatwa katika maeneo ya misitu wamekuwa
wakidai kuwa wana vibali vya uvunaji wa mazao ya misitu, kwa hiyo timu
hiyo itachunguza uhalali wa vili hivyo na mtoaji.
Bi
Galawa amesema amefikia uamuzi huo baada ya kushukudia uharibifu mkubwa
wa mazingira katika wilaya ya Handeni na kuwakamata watuhumiwa wawili
waliokuwa kwenye msitu wa Kang’ata wilayani humo wakiendelea na ukataji
miti ya uwoto wa asili.
“Tume
hiyo itachunguza nani ana kibali, kimetolewa na nani na cha muda gani”.
Amesema Bi Galawa na kuongeza kuwa kimsingi serikali haiwezi kukaa
kimya huku ikiona kuna baadhi ya wananchi wanaoharibu misitu na kuongeza
upotevu wa mvua.
Watuhumiwa
waliokamatwa na mkuu huyo wa mkoa kwa uharibifu wa misitu ni Abraham
Yameti(50) na Augostine Jacob(42) wote wakazi wa Kang’ata wilayani humo.
No comments:
Post a Comment