Kamishna wa Kazi Msaidizi, Bwana Josephat Lugakingira akitoa Tamko la Serikali kuhusu migomo sehemu za kazi jana jijini Dar es Salaam. |
Kwa mujibu wa kifungu cha 80(1) cha Sheria ya Ajira
na Mahusiano Kazini Na.6/2004 ili mgomo uwe halali ni budi mambo yafutayo
yazingatiwe:
- Ni lazima kuwepo na mgogoro wa maslahi baina ya wafanyakazi na mwajiri.
2:Mgogoro huo uwe umeishawasilishwa kwa kutumia fomu maalum katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi.
3:Mgogoro uwe haujapatiwa ufumbuzi baada ya siku thelathini (30) kupita tangu ulipopokelewa na Tume au katika muda wa siku thelathini za ziada zilizoongezwa na Tume.
4:Mgogoro uwe haujapokelewa na Tume au katika muda wa siku thelathini zilizoongezwa na Tume.
5:Mgomo uwe umeitishwa na Chama cha Wafanyakazi na kura imepigwa kwa mujibu wa Katiba ya Chama cha Wafanyakazi husika na wengi wa wanachama wawe wanaunga mkono.
6:Taarifa ya masaa arobaini na nane (48) itolewe kwa mwajiri ikielezea nia ya wafanyakazi kugoma.
Hata hivyo kwa mujibu wa kifungu
cha 76(1) cha sheria hiyo hiyo wafanyakazi walio katika huduma muhimu
hawaruhusiwi kugoma isipokuwa tu baada ya kukidhi vigezo kadhaa vinavyosimamiwa
na kamati ya huduma muhimu.
Kupitia gazeti la Mwananchi la
tarehe 09/07/2012 Chama cha Walimu Tanzania Wilaya ya Geita kimeazimia
kufanya mgomo usio na kikomo kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ni madai
ya muda mrefu.
Tayari Chama cha Walimu Tanzania
kimeishawasilisha mgogoro katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi – Dar
es Salaam wenye namba za usajili CMA/DSM.ILA/369/12 na Tume inaendelea
kuushughulikia.
Tunachukua fursa hii kuwataarifu
wafanyakazi wote kuwa migomo ambayo si halali inamadhara yake ikiwa
ni pamoja na kuchukuliwa kwa hatua za kinidhamu dhidi ya wahusika.
Mgomo uliozungumziwa kupitia gazeti
la Mwananchi ni BATILI. Hivyo Serikali inawataka wahusika wote
kutojihusisha na vitendo vya uvunjaji wa sheria na badala yake Sheria
na Kanuni zinazotawala mahusiano sehemu za kazi ziheshimiwe na kuzingatiwa.
09/07/2012
S.H. Kinemela
KAMISHNA WA KAZI
No comments:
Post a Comment