Meneja
wa Kinywaji cha Grand Malta Consolata Adam akifafanua jambo wakati wa
mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu mechi ya
kirafiki ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na timu ya watu
wenye ulemavu wa ngozi Albino United
utakaofanyika jumamosi mjini Dodoma na kudhaminiwa na TBL kupitia
kinywaji chake kisicho na kilevi cha Grand Malta. Kushoto ni Seif
Kulate, Said Ndonge na Mohamed Kindunyo.
Katibu wa timu ya Albino United, Mohamed Kindunyo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu pambano lao na Wabunge litakalofanyika mjini Dodoma siku ya Jumamosi.
NA MWANDISHI WETU
TIMU ya soka inayoundwa na watu wenye ulemavu wa ngozi Albino Albino
United wanatarajia kwenda mkoani Dodoma Ijumaa ambako watakwenda
kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Wabunge ambao wako mkoani humo kwa
shughuli za kibunge.
Akizungumza
jana katika Mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa
Idara ya Habari (MAELEZO) Katibu wa timu hiyo Said Ndonga amesema wana
uhakika kwamba watacheza katika kiwango.
Timu hiyo ambayo katika iliwahi kushiriki katika Ligi ya Shirikisho la Soka nchini TFF msimu uliopita na kufika katika ngazi ya Taifa Wilaya ya Ilala.
Safari na mechi ya Albino United imedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa kupitia kinywaji chake kisicho na kilevi cha Grand Malta.
Akizungumza katika mkutano huo mdhamini ambayeni
Meneja wa Grand Malta , alisema kwamba watatoa udhamini kwa wachezaji
20 tu kati ya 40 wanaounda timu hiyo ya Albino United kwa kuwasafirisha
chakula, malazi na posho.
No comments:
Post a Comment