Uongozi
wa Twiga Stars umekana kuwepo vitendo vyovyote vya kinyume na maadili
kwa wachezaji wa timu hiyo ambayo hivi karibuni ilitolewa kwenye mechi
za mchujo za michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC).
Wakizungumza
na waandishi wa habari leo, Meneja wa Twiga Stars, Furaha Francis, na
aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo Charles Boniface Mkwasa, wamesema
hakuna vitendo vya aina hiyo.
Mkwasa
amesema alikaririwa vibaya kuhusu suala hilo wakati akiwa kwenye
mahojiano na kituo cha televisheni cha Star Tv kutokana na swali
alilokuwa ameulizwa kuhusiana na vitendo hivyo.
“Ukifuatilia mahojiano yangu na Star Tv mimi sikusema kuwa kuna vitendo hivyo.
Tatizo
nadhani lilianzia kwa magazeti yaliyonukuu kupitia Star Tv, na wala
kujiuzulu kwangu hakukuhusiana na hilo, nimewajibika kama kocha kutokana
na kutolewa na Ethiopia,” amesema Mkwasa.
Naye
Furaha Francis amesisitiza kuwa hakuna vitu vya aina hiyo katika timu
hiyo, na kama kuna mtu ana ushahidi na hilo ni bora akauonesha badala ya
kuzungumzia uvumi kuliko ukweli.
“Ukweli
ni kwamba si sisi na wachezaji tu ambao hatukufurahishwa kutolewa na
Ethiopia, wapo Watanzania wengi ambao hawakufurahishwa na matokeo yale.
Twiga Stars si timu ya kudumu, haikai na wachezaji kwa muda wote, kila mchezaji ana timu yake.
“Madai yanayoenezwa na baadhi ya vyombo vya habari kuhusu vitendo hivyo yametuchafua sana.
Tunaomba kama kuna mtu ana ushahidi na hilo atueleze kuliko kuendelea kutuchafua,” amesema.
No comments:
Post a Comment