JUMLA ya
warembo 15 wamejitokeza kuwania taji la
Mrembo wa Sinza “Redds Miss Sinza 2012” yaliyopangwa kufanyika julai 13 kwenye
ukumbi wa Mawela social (Ten Star Lounge)
uliopo karibu na hotel ya Vatican City.
Mratibu wa
mashindano hayo, Majuto Omary wa kampuni ya Calapy Entertainment aliwataja
warembo hao kuwa ni Mariam Miraji, Naima Mohamed, Lulu Ambonela, Maria John,
Eva Mushi, Vailet John, Esther Mussa, Christina Samwel, Nahma Said, Shadya Ali,
Aisha Ramadhan, Nancy Musharuzi, Brigitter Alfred na Merina Mushi.
Majuto alisema
kuwa warembo hao wapo kambini chini ya mwalimu wao, Mwajabu Juma ambaye kwa
sasa anashikilia taji la Miss Tanzania Top Model. Alisema kuwa mazoezi ya
warembo hao yanafanyika kwenye ukumbi wa mashindano hayo, Mawela social kuanzia
saa 8.30 mchana.
“Warembo
wamepania kufanya kitu cha kihistoria siku ya mashindano nah ii inatokana na
ukweli kuwa wamejiandaa vilivyo na kwa sasa wanamalizia tu baadhi ya vitu
vidogo vidogo vya mashindano hayo, alisema Majuto.
Alisema kuwa
lengo kubwa la mashindano ya mwaka huu ni kutwaa taji la Redds Miss Tanzania
mbali ya taji la Kanda ya Kinondoni katika shindano hilo lililodhaminiwa na
Redds Premium Cold, Dodoma Wine, Kidoti Fashion, Clouds Entertainment, sufianimafoto.blogspot.com,
Lady Pepeta na flexi P, Fredito Entertainment, Screen Masters, Brake Point na Jackz Cosmetics Kinondoni.
“Tuna
warembo moto wa kuotea mbali ambao kwa sasa wameonyesha kupania kufanya kile
ambacho kimesubiliwa na wadau wa warembo wa mitaa ya Sinza na vitongoji vyake,
hii inatokana na ukweli kuwa mashindano haya ni ya mwisho kwa upande wa
vitongoji jijini,” alisema.
No comments:
Post a Comment