Saturday, July 28, 2012

YANGA WALIVYO KINUKISHA UWANJA WA TAIFA LEO. WAKATAA LAMBALAMBA ZA BAKHRESA. Mfupa uliomshinda Simba waula kiulainiiii


Mshambuliaji wa yanga Said Bahanunzi akimtoka beki wa Azam FC Agrey Morris wakati wa mchezo wao wa Fainali ya Kagame Cup uliomalizika hivi punde kwenye uwanja wataifa jijini Dar es Salaam ambapo Yanga wameibuka na Ushindi wa mabao 2-0, huku Bahanuzi akipachika bao kwenye dakika za nyongeza za mwamuzi.
Mshambuliaji wa Yanga Hamis Kiiza Akimtoka Beki wa Azam Fc Jabir Azizi kabla ya kupachika bao la kwanza kwenye mchezo huo.
Mashabiki wa Yanga wakijimwayamwaya kwenye uwanja wa Taifa leo baada ya Said Bahanuzi kupachika bao la pili.
Wachezaji nao waliburudika kimtindo baada ya kupata ushindi.

No comments:

Post a Comment