Monday, August 27, 2012

AIKAROSE MWASHA MTOTO WA KITANZANIA ANAYENG'ARA NA MCHEZO WA TAEKWANDO JIJINI BELGIUM


 AikaRose Mwasha (kulia) akiwa na Medali yake na mchezaji mwenzake.

NYOTA TUMAINI LETU
Jina: AikaRose Mwasha
Jinsia:Kike
Miaka:12
Utaifa:TANZANIA
Mchezo: Taekwando 
KILO: 28 kg- beginners FEMALE
Club: Nong Jang
Makazi: Leuven Belgium
MAFANIKIO: MEDALI YA FEDHA & DHAHAB
*************************************
Kijana wa kitanzania mwenye ndoto ya kuwakilisha nchi yake kwenye mashindano ya kimataifa siku za usoni kwa kupitia mchezo wa mbinu za kujihami wa TAEKWANDO ,anamapenzi makubwa na mchezo huo aliouanza tangu akiwa mdogo na umri wa  miaka 9 , na hadi sasa ameshashiriki mashindano madogo madogo nchini Belgium na kupata mafanikio makubwa kufikia medali ya fedha. 

Hivi karibuni alifanikiwa kupata medali ya dhahabu katika mashindano ya Olympic open Brussels yaliyofanyika Rue Du Lombartzyde Brussels Belgium tarehe  27 May 2012.

Sasa hivi anajiandaa na team yake kwenda Copenhagen kwenye  mashindano ya Wonderfull Copenhagen yatakayofanyika mwezi ujao.

Wito wake hasa kwa vijana wadogo akitilia mkazo jinsia ya kike ni kujifunza michezo mbalimbali na kuwa na ndoto ya kuwa mabalozi kwa taifa lao la TANZANIA, VIPAJI HUINUA TAIFA
 AIKAROSE, AKIPOZI WAKATI WA MAZOEZI YAKE YA KUJIANDAA NA MOJA KATI YA MECHI ZAKE ALIZOISHA CHEZA.
 AIKAROSE, AKIWA KATIKA MAZOEZI NA KOCHA WAKE.
AIKAROSE, AKIPOZI KWA PICHA NA FANS WAKE.

No comments:

Post a Comment