Monday, August 13, 2012

Bondia wa kike,Lulu Kayege ajifua kwa ajili ya kuwakabiri wapinzani wake


Kocha wa Mchezo wa ngumi Kambi ya Ilala Habibu Kinyogoli akimfundisha bondia chipkizi wa kike,Lulu Kayege Dar es salaam leo  .kwa ajili ya kujiandaa na mipambano yoyote itakayoshirikisha wanamasumbwi wa kike picha na www,superdboxingcoach.blogspot.com
 

Kocha wa Mchezo wa ngumi Kambi ya Ilala Habibu Kinyogoli akimfundisha bondia chipkizi wa kike,Lulu Kayege Dar es salaam leo  .kwa ajili ya kujiandaa na mipambano yoyote itakayoshirikisha wanamasumbwi wa kike picha na www,superdboxingcoach.blogspot.com

 Kocha wa Mchezo wa ngumi Kambi ya Ilala Kondo Nassoro akimfundisha bondia chipkizi wa kike,Lulu Kayege Dar es salaam leo kwa ajili ya kujiandaa  na mashindano ya kumi bora yatakayofanyika june 15 katika ukumbi wa panandi panandi Ilala Bungoni Dar es salaam.picha na www,superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia wa kike,Lulu Kayege akiwa katika pozi bondia huyo  anaenolewa katika Kambi ya Ilala na Makocha wazowefu wa mchezo wa Masumbwi Nchini Habibu Kinyogoli 'Masta, Rajabu Mhamila 'Super D' na Kondo Nassoro kwa sasa yupo fiti kwa ajili ya masindano mbalimbali nchiniwww,superdboxingcoach.blogspot.com

Na Mwandishi Wetu Kambi ya Ilala

BONDIA wa Kike Lulu Kayage yupo katika mazoezi mazito katika kambi ya ngumi ya Ilala Inayuongozwa na Kocha Mkongwe Habibu Kinyogoli 'Masta' na Kocha wa kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super D' pamoja na Kondo Nassoro na Sako Mtlya

Akizungumzia mchezo wa masumbwi ulivyomfutia mpaka kuasnza mazoezi katika kamhi hiyo aslisema chezo anaupenda na pia unamjenga kiafya na ki mwili kwani amekuwa akishiriki mazoezi tangia mwezi April mwaka huu na maendeleo yake ni mazuri akiwa chini ya uwangalizi wa makocha wake hawo

Bondia huyo wa kike aliyezaliwa 1990 anamatarajio makubwa ya kuwa ingwa wa dunia katika masumbwi ususani upande wa wanawake 

bondia huyo anaye vutiwa na uchezaji wa mkongwe wa masumbwi nchini Rashidi Matumla 'Snake Man'  ambapo kwa nje anavutiwa na mabondia toafauti ambapo mmoja wapo ni Mbunge wa Filpino Manny Paquaio na bondia asiyepigika ambaye kwa sasa anatumikia kifingo cha siku 90 kwa kosa la kumshambulia aliyekuwa mpenzi wake na mama watoto wake
Katika mazoezi anayofanya na kambi ya Ilala ambayo wanawake wapo wawili ambapo anaendelea kujisikia faraja kwa kuwa wapo katika mazoezi pamoja kama ndugu na nidhamu ya ali ya juu iliyopo hapo katika kambi hiyo

aliwataka wanawake wajitokeze katika mchezo wa masumbwi kwani ni mchezo kama michezo mingine ambapo ata ukiangalia mchezo watu wanapopigana wakimaliza wanakubatiana kwa furaha ni kwa ajili ya kutambua mchezo wa masumbwi si uadui bali ni mchezo


Vikwazo ambavyo amewai kukutana navyo ni pamoja na kukatishwa tamaa kwa watu ambao awapendi michezo kwani wanasema mwanamke mzima unacheza ngumi uogopi kutolewa manundu kuaribiwa sura ehee uzuri wote huo hizo ni sehemu tu za watu wasiopenda michezo kwani kuna vikwazo
 vingi ambavyo tuna vipata mabondia wa kike 

kwa mara ya kwanza nilipotokea kwenye magazeti tu watu walinifata na kunishauli niachane na mchezo lakini kwa sasa nimeshaiva na nipo tayali kwa mapambano mbalimbali yatakayojitokeza

kwa kuwa mimi ni bondia bora pekee wa kike nchini na ninaetoka katika kambi bora kabisa ya mchezo wa masumbwi nchini naisi cheche zangu mtaanza kuziona mwazi agost kwa kuwa kwa sasa nipo kwenye mazoezi makari ambayo yananipa uwezo wa ali ya juu katika masumbwi 

Aliongeza kuwa kwa kufundishwa na kocha wa kimataifa Super D anaefundisha mafundisho hayo kupitia DVD zake ambazo  amechanganya na clips za mabondia mabingwa wa dunia akiwemo Manny Paquaio,floyd Mayweather, Roy Jones, Mohamedi Ali, Mike Taysoni na wengine ameziona na kuzifanyia kazi ambapo kwa sasa anajua mbinu za Ndani na nje ya nchi kutokana na Supe D kumpatia uwezo wa kina katika maswala ya mchezo wa Masumbwi Duniani

Katika mchezo uhu siwezi kukata tamaa katika mazoezi na nawambia mashabiki wa mchezo wa masumbwi watarajie mafanikio yangu katika masumbwi

No comments:

Post a Comment