Friday, August 24, 2012

CCM bado kina nguvu kubwa - Kigwangalla


Mbunge wa Nzega, Hamis Kigwangalla, akichukua fomu ya kuwania Uenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa leo kutoka kwa Katibu wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Mwanza, Habiba Haji. (Picha zote na Baltazar Mashaka)


Mbunge wa Nzega, Hamis Kigwangalla, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania Uenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa leo.



Na Baltazar Mashaka,MWANZA

MBUNGE wa Jimbo la Nzega (CCM) Hamis Kigwangalla (39), amechukua fomu kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, akisema kuwa chama hicho hakijapoteza mvuto kwa wananchi kama inavyodaiwa bali bado kina nguvu kubwa.
Alisema CCM haijapoteza mvuto, bado kina nguvu kubwa, ndiyo sababu kimeendelea kuchanguliwa na wananchi na kuiwezesha kushika dola ikiwa ni pamoja na kupata asilimia 78 ya wabunge wote wa Tanzania.

Alisema CCM inakabiliwa na changamoto nyingi kutoka kwa wapinzani,ambazo zinakifanya kishindwe kujipambanua katika misingi yake na kujikita kukabiliana na changamoto hizo za ushindani wa kisiasa.

Changamoto ni jambo la kila siku, ushindani upo na wenzetu wanajipanga na sisi pia.Wanatuchelewesha na kutukwaza kuwaletea wananchi maendeleo.Katika nchi dhalimu, hilo lisingetokea,wabunge wawili wa chama tawala kutenguliwa kunaonyesha kuna haki na maadili katika mahakama zetu na haya yanaletwa na CCM îalisema Kingwangalla.

Alitoa kauli hiyo jana Jijini Mwanza,alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi taifa, mara baada ya kukabidhiwa na Habiba Haji, Katibu wa Jumuiya hiyo mkoa wa Mwanza. 
Kuhusu mpasuko ndani ya chama hicho tawala alidai ni ya kawaida,lakini akaenda mbali zaidi kuwa hata Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF naako kuna mpasuko kuliko CCM.

Mipasuko ni ya kawaida,yipo la chama si CCM tu , na si jambo la ajabu.Kwa nini CCM tu ndiyo inasemwa ina makundi.Kisiasa makundi ni lazima yawepo wakati wa uchaguzi,ukiisha tunakuwa kitu kimoja, alisema.
 
Alisema maadui wa Watanzania ni watatu tu, ambao ni maradhi, ujinga na umasikini na si vyama, hayo ndiyo yanapaswa tutafute njia ya kuyakabili ili kufikia mabadiliko ya kweli.
Mbunge huyo wa Nzega alijibodoa kuwa msafi na hajawahi kutuhumiwa kwa rushwa wala ufisadi na ni mmoja wa watu wanaouchukia ufisadi,kwa sababu unakwamisha juhudi za kuwaletea maendeleo wananchi.

Ufisadi ni adui yangu, unatukwamisha kufikia malengo na kuleta mabadiliko ambayo wananchi wanayahitaji.Kwa sasa watu wanashabikia siasa na kusahau kufanya kazi.Naamini sera na mikakati ya CCM haijaanguka na bado naamini zinafanya kazi vizuri,îalisema na kuongeza; 

Naamini nitashinda, sifa ninazo, jumuiya ya wazazi ndiyo inayotengeneza jumuiya zote tatu za CCM.Mimi ni kada mzuri ninayeamini katika mabadiliko ili kupata viongozi wazuri wanaoendana na hali ya sasa.Nitatumia ubunifu, elimu yangu na uzoefu wangu katika siasa kuleta mabadiliko wanayohitaji wananchi. Alisema Mbunge huyo wa Nzega.

Alisema uongozi si kuwa na mvi bali nia thabiti na uwezo wa kuona mbali katika kutatua changamoto za unaowatumikia,hivyo anaamini ndani ya CCM,bado kuna watu wasafi wenye nia thabiti ya kuwatumikia wananchi tofauti na inavyodaiwa na wapinzani.

Alisema miradi mingi ya jumuiya hiyo imefisadiwa na viongozi, akiwa kiongozi wa jumuiya hiyo lazima ahakikishe rasilimali zilizopo zinawanufaisha wote na kusisitiza, yeye ni mtu safi na hajawahi kutuhumiwa kwa rushwa,hivyo atasimamia misingi ya chama chake tangu kilipoasisiwa.

Kigwangalla alisistiza kuwa akichaguliwa kushika wadhifa huo wa juu katika jumuiya hiyo atahakikisha anatumia uzoefu na elimu yake kuleta mabadiliko yanayohitajika kwa wananchi.

Mbali na Kingwangalla, tayari kada na mmoja wa walezi wa jumuiya ya Wazazi mkoa wa Mwanza, John Lema amechukua fomu, pia akiwania kiti hicho.Lema alichukua fomu hiyo mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment