Tuesday, August 21, 2012

CCM YAKANUSHA KAULI YA CHADEMA YA KUINGIZA SILAHA NCHINI


 Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye, akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Nape amezungumzia maswala kadhaa ikiwemo CCM kukanusha madai ya Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Wilbrod Slaa aliyoitoa juzi mjini Morogoro kwamba CCM imekuwa na utaratibu wa kuingiza silaha nchini kinyemela. Picha na Bashir Nkoromo
**************************************
''Dk. Slaa Anazeeka vibaya'', Nape
KATIBU  wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Nape Nauye amemshukia Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, kufuatia kauli aliyoitoa mkoani Morogoro kwamba Chama Cha Mapinduzi kimekuwa kikiingiza silaha nchini.

"Kauli hii inaonyesha ni vipi Dk. Slaa ameanza kuzeeka vibaya, na sasa kazi ya siasa inamshinda hivyo awaachie vijana" alisema Nape na kuongeza kwamba anatambua kuwa uzee siyo laana kama unamwingia mtu vizuri.

Akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, Nape amesema, mbali na kuzeeka vibaya, hatua ya Dk. Slaa kuizushia CCM kwamba imekuwa ikiingiza siala kinyemela ni dalili kwamba ameona kuwa sasa operesheni ya mikutano ya Chadema hasa ya Morogoro zinazorota.

Kwa mujibu wa Nape, Dk. Slaa amesikika akitangaza mjini Morogoro kwamba, CCM imekuwa ikiingiza siala nchini na kuwapa vijana wazitumie wawapo kwenye makambi ya Umoja wa Vijana wa CCM.

"Kwanza huyu Mzee inaonyesha ni jinsi gani ufuatiliaji wake wa mambo ni vinyu, kutoa madai kwamba tumeagiza siala kinyemela kwa ajili ya makambi ya vijana wetu, wakati inafahamika kwamba wakati huu CCM imo katika uchaguzi mkuu hatuwezi kabisa kuandaa wala kufanya makambi ya vijana", alisema Nape.

"Kutokana na kauli hizi za uzushi, tunazitaka mamlaka zinazosimamia ulinzi na usalama kumtaka Dk. Slaa awapatie ushahidi wa kina kuhusu mtu au tasisi yoyote ambayo inaingiza silaha nchini kinyemela, na kama ushahidi wake utawezesha kupatikana yeyote basi ashughulikiwe kwa mujibu wa sheria", alisema.

"Huyu Mzee imekuwa kawaida yake kuandaa uongo kila anapoona kwamba anakabia kushindwa katika operesheni au mipango yake au ya Chama chake kisiasa. Wakati ule wa Uchaguzi mkuu, alipoona kwamba atashindwa, alizusha kwamba CCM imeingiza kura nchini kutoka nje ya Nchi, lakini ikabainika kuwa ni uzushi", alisema.

Alisema, hatua ya Dk. Slaa kuzusha uongo ni njama ya kuandaa fujo zitakazofanywa watu walioandaliwa na Chadema, kufanya fujo mitaani wakati wa mikutano wa chama hicho mkoani Morogoro. " sasa anatoa uongo huu, ili watu wao waliokusanya watakapofanya fujo azushe kwamba ni vijana waliotumwa na  CCM".

No comments:

Post a Comment