Tuesday, August 21, 2012

MISS WORLD TANZANIA LISA JENSEN AREJE KUTOKA CHINA


Mrembo Lisa Jensen ambaye ni Miss World Tanzania 2012, akizungumza na Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,  jijini Dar es Salaam jana jioni akitokea nchini China alipokwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya urembo ya Dunia mwaka huu na kupokelewa na viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania.
Lisa, akizungumza na viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania, kutoka kushoto, Katibu Mkuu, Bosco Majaliwa, Mrembo Amisa Hassan, Mkurugenzi Hashim Lundenga na Ofisa Habari wa Kamati, Haidan Rico.
Lisa akipozi kwa picha na mmoja kati ya warembo waliofika kumpokea Amisa Hassan. Lisa alifanikiwa kuingia Robo fainali za Top Model na kumi na bora ya Shindano la Multmedia Award 2012.

No comments:

Post a Comment