Friday, August 17, 2012

EXTRA BONGO WAFUTURU NA WATOTO YATIMA



 

Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo akifuturu pamoja na Watoto yatima wa kituo cha kulelea watoto hao cha New Life kilichopo Kigogo jijini Dar es Slaam
Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Choki wakiwa na Mkurugenzi wa kituo cha Kulele Watoto Yatima cha New Life
Na Michael Machellah
BENDI ya Muziki wa Dansi ya Extra Bongo leo imefuturu pamoja na Kituo cha Watoto Yatima cha Home New Life kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Chocky amesema wamefanya hivyo ili kuonyesha upendo kwa watoto hao ambao pengine kwa kipindi kama hiki wangekuwa na Wazazi wao lakini kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu wako katika mazingira hayo na si kwa ridhaa yao.
Alisema Chocky wao kama sehemu ya jamii inayowazunguka watoto hao hawanabudi kufanya hivyo angalau hata Watoto hao nao wajitambue kuwa kana jamii inawazunguka na inatambua uwepo wao.
Chocky alisema kwa mfano huo anawaomba hata Bendi zingine waige mfano huo na si bendi tu bali hata watu binafsi kwani Watoto hao ni wetu sote hatuna budi kuwafariji na kufurahi pamoja nao tupatapo nafasi.
Bendi ya Exta Bongo sasa iko kwenye mazoezi makali ikijiandaa na maonyesho ya Idd mosi na Idd pili ambapo Idd mosi wanatarajia kufanya onyesho katika Ukumbi wao wa New White Kimara na Idd pili watakuwa katika Ukumbi wa Meeda Sinza jijini Dar es Salaam.
Watoto Yatima wa kituo cha New Life wakifuturu pamoja na wanamuziki wa Bendi ya Extra Bongo
Mwimbaji wa Bendi ya Extra Bongo, Rama Pentagon akigawa maadazi kwa watoto wakati wa futari hiyo

No comments:

Post a Comment