Sunday, August 12, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AHUDHURIA FAINALI ZA MASHINDANO YA KIMATAIFA YA QUR-AN


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakati alipowasili kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo Agosti 12, 2012 kuhudhuria fainali za mashindano ya kimataifa ya Qur-an yaliyoshirikisha nchi 13, ambapo mshindi alikuwa ni Abdulrahman Salis Ahmad (18) kutoka Nigeria, aliyeshinda kwa jumla ya Pointi 96.12. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
 Mmoja kati ya washiriki wanne walioiwakilisha Tanzania, katika fainali za mashindano ya kimataifa ya Qur-an, yaliyoshirikisha nchi 13, Omar Abdallah, akisoma Qur-an wakati akishiriki katika fainali za mashindano hayo ya Kimataifa yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam leo Agosti 12, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati alipohudhuria na kuwa mgeni rasmi katika fainali za mashindano ya Qur-an ya kimataifa, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee leo Agosti 12, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya Dola za Kimarekani 1250, mshindi wa tatu katika fainali za mashindano ya Kimataifa ya Qur-an, Ijaaz Mukaddam (22), kutoka Afrika ya Kusini, aliyepata jumla ya Pointi 95.08 baada ya kutangazwa washindi wa fainali hizo. Mshindi wa kwanza alikuwa ni Abdulrahman Salis Ahmad (18) kutoka Nigeria, aliyepata Pointi 96.12, wa pili ni Twalha Ally Mohammed (18) kutoka Philippines, aliyepata Pointi 96.03. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi funguo ya Pikipiki, mshindi wa kwanza kwa watanzania, Mohammed Omar Mkilalu, baada ya kutangazwa washindi wa fainali za mashindano ya Kimataifa ya Qur-an, zilizofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam leo Agosti 12, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na mshiriki mdogo kuliko wote katika mashindano hayo ya Qur-an, ya kimataifa, Suleyman Ahmad (9) kutoka China, aliyeshiriki katika fainali hizo zilizofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee leo Agosti 12, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti Ustaadh Muhammad Abdullah Balarabe, aliyeongozana na mshiriki mshindi wa kwanza katika fainali za mashindano hayo ya Kimataifa ya Qur-an, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee leo Agosti 12, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Taasisi za Dini ya Kiislamu na washindi wa tatu Bora wa fainali za mashindano ya Kimataifa ya Qur-an, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee leo Agosti 12, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa fainali za mashindano ya Kimataifa ya Qur-an, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee leo Agosti 12, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment