Friday, August 24, 2012

MASUMBWI WAUNGA MKONO MPANGO WA TFF KUWEKA SHERIA ZA KUDHIBIBIRI WACHEZAJI WANAOTUMIA DAWA ZA KULEVYA



NDG WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO ,

HIVI KARIBUNI RAIS WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU NCHINI TANZANIA [TFF] NDG LEODGER CHILA TENGA ,ALINUKULIWA NA VYOMBO VYA HABARI KARIBU VYOTE VILIVYOKO NCHINI TANZANIA ,AKITOWA MAELEKEZO KWAMBA SASA TFF IKO MBIONI KUANZA KUWADHIBITI WACHEZA MPIRA WA MIGUU WA NCHI HII YA TANZANIA WANAOTUMIA MADAWA YA KULEVYA HUSUSAN BANGI, GANJA, HASHISHI ,NA HATA NDUMU- KAMA WATUMIAJI WENYEWE WANAVYOIPAMBA KWA MAJINA HAYO HUKO MITAANI.
UAMUZI WA RAIS HUYU MUADILIFU WA TFF UNAPASWA KUPONGEZWA NA VIONGOZI WA MICHEZO WOTE KATIKA NCHI HII YA TANZANIA ,HASA KWA KUZINGATIA HATIMA YA WACHEZAJI WAVUTA BANGI MARA WATAKAPOKUWA WAMEFILISIKA UWEZO WA VIWANGO VYAO ,NA WATAKAPOKUWA NJE YA UWANJA KAMA WATAZAMAJI WA KAWAIDA .
NINAO USHAHIDI WA KUTOSHA KWAMBA WAPO BAADHI YA WACHEZAJI WA ZAMANI NA WALIKUWA NI WAZURI MNO AMBAO MPAKA HIVI SASA WAMEPOTEZA MUELEKEO BAADA YA KUWA NJE YA MPIRA WA MIGUU NA WALIKUWA WAKIVUTA HIZO BANGI NA SASA WAMEKUWA WATU WA VIJIWENI WAKIENDELEZA TAALUMA YA KUVUTA HIZO BANGI AU HATA KUWA WAUZAJI KAMA WAVUTAJI WENYEWE WANAVYOWAITA -  [MAPUSHER-MEN ].
ORGANAIZESHENI YA NGUMI ZA KULIPWA TANZANIA [TPBO ] INAAMINI KABISA KWAMBA VITA VYA KUPAMBANA NA MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA NA HATA YA KUONGEZA NGUVU MICHEZONI HAVIHITAJI MANENO MATUPU BALI VINAHITAJI USHUJAA MKUBWA NA UWAZI KATIKA UTEKELEZAJI WAKE ,HIVYO RAIS WA TFF ANAHITAJI AWE NA MADAKTARI WENYE UAMINFU NA AMBAO HAWATAKUWA TAYARI KUSHAWISHIWA KWA LOLOTE ILI WAPINDISHE TARATIBU WATAKAZOELEKEZWA.
HII IKIWA NA MAANA KWAMBA KABLA YA KUABNZA KWA MECHI ZA KILA SIKU ZA LIGI WACHEZAJI WOTE HUSIKA NA MECHI HIYO WAPIMWE MKOJO NA DAKTARI NA BAADA YA MECHI WAPIMWE TENA MKOJO NA DAKTARI ,HII IKIWA NA MAANA KWAMBA WAKIPMWA ASUBUHI PEKEE INAWEZA KUTOWA MWANYA WAKATI WA MAPUMZIKO WAKAINGIA VYOONI NA KUVUTA TENA .HIZO BANGI.
TPBO IMEKUWA MSTARI WA MBELE SANA KTK KUPIGA VITA MATUMIZI YA MADAWA YA KUONGEZA NGUVU NA YA KULEVYA HASA BANGI NA TUMEKUWA TUKITOWA MSIMAMO WETU HADHARANI BILA WOGA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI ,NA HAPO MWANZO ILIKUWA NI KAZI NGUMU LAKINI KWA KUWA NI MOJA YA KANUNI KTK NGUMI ZA KULIPWA KOTE DUNIANI HATIMAYE MABONDIA WAMEIZOWEA HALI YA KUPIMWA KABLA NA BAADA YA MAPAMBANO YAO.
NINARUDIA TENA KUMPONGEZA RAIS WA TFF NDG TENGA KWA MTAZAMO WAKE HUU MPYA AMBAO NIADHANI UTAPUNGUZA KWA KIASI KIKUBWA SANA UTOMVU WA NIDHAMU WA NDANI NA NJE YA UWANJA ,NA HATA SHERIA NA KANUNI ZA MPIRA WA MIGUU ZITAZINGATIWA NA PIA HATA USALAMA WA WAAMUZI UTAIMARIKA  HAWATAPIGWA NA WACHEZAJI. NA HESHIMA YA MPIRA ITAIMARIKA SANA SANA.
NINATUMIA FURSA HII KUWATAKA PIA VIONGOZI WA VILABU VYA MPIRA WA MIGUU KOTE NCHINI TANZANIA KUMPA USHIRIKIANO MKUBWA SANA RAIS WA TFF KATIKA VITA HII YA KUPAMBANA NA MADAWA YA KUONGEZA NGUVU NA KULEVYA KATIKA MCHEZO UNAOPENDWA NA WENGI NCHINI -MPIRA WA MIGUU.NA WAWE TAYARI KUZIPOKEA ADHABU WATAKAZOPEWA WACHEZAJI WAO MARA WAKITHIBITIKA KUWA NA MAKOSA HAYO.
NA NJIA AMBAYO VIONGOZI WA VILABU WANAWEZA KUFANYA KWA KUSHIRIKIANA NA TFF NI KUWAPA SEMINA WACHEZAJI WAO MARA KWA MARA JUU YA HATARI YA MADHARA YA MADAWA YA KULEVYA KWA WANAMICHEZO KWA KUWATUMIA WATAALAMU WALIOBOBEA KATIKA KUELIMISHA WANANCHI HATARI ZITOKANAZO NA MATUMIZI YA MADAWA HAYO.



MUNGU IBARIKI TANZANIA , NA WATU WAKE WOTE 



MUNGU WAEPUSHE WANAMICHEZO WOTE WA TANZANIA NA MATUMIZI YA BANGI MICHEZONI.



MUNGU UWAJAALIYE WACHEZAJI WOTE WANAOVUTA BANGI WAACHE KABLA HAWAJAFEDHEHESHWA NA VIPIMO. AMEEEEEEN




                       IMEANDIKWA NAMI;-
               YASSIN ABDALLAH -USTAADH
           RAIS- TANZANIA PROFESSIONAL BOXING ORGANISATION--TPBO

No comments:

Post a Comment