Friday, August 24, 2012

VERONICA MPANGALA ATWAA TAJI LA ‘BIBI BOMBA 2012’


Mshindi wa shindano hilo, Veronica Mpangala akiwa amebebwa juujuu na shabiki wake.

SHINDANO la ‘Bibi Bomba’ ambalo lilikuwa likiratibiwa na kituo cha Clouds TV, usiku wa kuamkia leo limefikia tamati na Veronica Mpangala akiibuka mshindi wa kitita cha 5,000, 000/= (milioni tano) huku nafasi ya pili ikitwaliwa na Anna Saidi ambaye alijipatia kiasi cha shilingi milioni tatu, na ukurasa wa washindi ukifungwa na Nasra Mohamed ambaye alijitwalia kiasi cha shilingi milioni moja na nusu.
Washiriki wengine watano ambao walikuwa wamesalia kwenye shindano hilo walipatiwa zawadi kila mmoja na watu mbalimbali waliokuwa wamealikwa kwa ajili ya kufanikisha zoezi hilo.
  Akiongea machache baada ya ushindi huo.
   
  Mkuu wa kitengo cha Habari wa kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, Arnold Madale (kulia), akimkabidhi zawadi Anna Saidi. Katikati ni aliyekuwa mshereheshaji shindano hilo, Babu wa Kitaa.
Msanii wa filamu, Jacob Steven ‘JB’ (kulia), akimkabidhi zawadi mshindi wa tatu, Nasra Mohamedi.
Mwanamuziki , Abubakari Chende ‘Dogo Janja’, akimkabidhi zawadi mmoja wa washiriki.
Mtangazaji wa Kipindi cha XXL cha Clouds FM, Fatuma Hassan ‘DJ Fetty’ (kulia), akiongea jambo kabla ya kukabidhi moja ya zawadi kwa washiriki hao.
DJ Choka (kulia), akimkabidhi zawadi mmoja wa washiriki.
Msanii wa filamu, Steven Mangele ‘Steve Nyerere’, akikabidhi moja ya zawadi kwa mshiriki.
Baadhi ya waandaaji wa shindano hilo wakitambulishwa kwa wageni waliofika hapo.
Mmoja wa wakurugenzi wa Clouds Media Group, Rugemalila Mtahaba ‘Ruge’, akisalimiana na mmoja wa Mabibi Bomba.
Baadhi ya mashabiki wakiserebuka baada ya mshindi kutajwa.

No comments:

Post a Comment