Mwanamitindo Remtula akiwa katika pozi tofauti.
Na Andrew Chale
Mwanamitindo
maarufu hapa nchini Ally Rehmtullah ameandaa onyesho kubwa na la
kipekee la mitindo hapa nchini litakalofanyika tarehe 8 Mwezi ujao
katika jiji la Dar es Salaam na litarushwa moja kwa moja katika mtandao
wa www.ar.co.tz bure kabisa ambapo atazindua rasmi kazi zake mpya za mitindo ya mavazi mbalimbali kwa wanaume na wanawake.
Akizungumza
na vyombo mbalimbali vya habari hivi karibuni, Rehmtullah alisema
dhumuni la kuandaa onyesho hilo la kipekee ni kuweza kuonyesha aina mpya
ya mitindo ya mavazi aliyobuni hivi karibuni na harakati zake za kuinua
kiwango cha kazi za mitindo ndani ya nchi.
“Nimepania
kupanua wigo wa taaluma ya mitindo na mavazi hapa nchini ili kazi za
wanamtindo na wabunifu wa mavazi hapa nchini ziweze kupenya kwenye soko
la ndani na la Afrika mashariki na ya kati wakati tayari kuna soko la
pamoja katika jumuiya ya Afrika mashariki,’ alisema.
Rehmtullah
alisema kwamba onyesho hilo litakuwa la kipekee kwa sababu mavazi na
onyesho litapambwa na rangi nyeupe,ubunifu wa hali ya juu pamoja na
muonekano mpya wa mavazi yaliyofanyiwa utafiti mkubwa ili kuweza
kuendana na utamaduni wa mwafrika.
Alisema
onyesho hilo ambalo litafanyika katika hoteli ya Serena litapambwa na
wasanii mbalimbali wa muziki na wacheza shoo toka sehemu mbalimbali hapa
nchini.
Rehmtullah
alisema onyesho hilo itakuwa ni nafasi ya kipekee kwa yeye binafsi
kuonyesha muonekano mpya wa tasnia ya mitindo hapa nchini na nje ya
nchini ili kuonyesha ni kwa jinsi ngani wanamitindo wa kitanzania
wanavyoweza kuonyesha kazi zao.
Alisema
kuwa tasnia ya mitindo kwa ujumla ina nafasi ya kipekee kwa wanamtindo
chipukizi hapa nchini kujitokeza na kuonyesha kazi zao kwa watu
mbalimbali hasa washika dau katika sekta hiyo.
‘kazi
za mitindo na mavazi ndio mkombozi wa kweli katika kupunguza tatizo la
ajira nchini Tanzania kwa sababu ni sekta inayokua kwa kasi kubwa na
inatoa ajira kwa vijana wengi wa kike na kiume,’aliongeza
Onyesho
hilo linategemewa kuhudhuriwa na watu zaidi ya 400 wakiwemo viongozi
mbalimbali kama mawaziri, wabunge, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa
mashirika mbalimbali.
Onyesho hilo litakuwa ni la mialiko maalum na limepewa jina la Ally Rehmtullah 2013 collection.
Wadhamini
wa onyesho hilo ni Mercedez Benz, Belvedere Vodka, DULUX, RAHA, HUGO
DOMINGO,THE Tanzanite Experience, Shiva Images, Farm Plant, Creative
Infinities, Out Door, Stanbic Bank, Phoenicia Properties, Dar es Salaam
Serena Hotel, Missie Popular Blog, Mo Blog, Quality Furniture na Mx
Carte
No comments:
Post a Comment