Wednesday, August 15, 2012

SAMSUNG YATANGAZA KUTOA MSAADA WA MILIONI 144 MONDULI


Mwenyekiti wa Kijiji cha Emairete, Moran Poyoni akimkabidhi zawadi ya fimbo maalumu Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Samsung, Choi Woo-Soo wakati wa hafla ya kukabidhi madarasa kwa shule ya Irmorijo yaliyokarabatiwa na Kampuni la Samsung na kutangaza msaada wa milioni 144 kwa shule hiyo na Sekondari ya Winning Sprit Monduli Arusha
Wamasai wa Kijiji cha Emairete Wilayani Monduli Arusha, Wakimpokea Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Samsung, Choi Woo-Soo aiyeambatana na Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Joika Kasunga wakati wa kuwasili katika Shule ya msingi ya Irmorijo kwa hafla ya kuabidhi madarasa yaliyokarabatiwa na Kampuni ya Samsung kutangaza kutoa msaada wa milioni 144 sawa na dola za kimarekani 90,000 kwa ajili ya kusaidia shule ya Msingi ya Irmorijo na Secondari ya Winning Spirit za Wilani Monduli Arusha
Wakiwasili kwa mapokezi
Wakiwasili katika Shule ya Msingi Irmorijo Monduli
Makamu wa Rais wa Samsung, Choi Woo-Soo(katikati), Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Joika Kasunga na Diwani wa Kata ya Monduli juu, Bariki Sumuni wakishangilia mara baada ya kukata utepe kwa pamoja kuashira uzinduzi wa madarasa yaliyokarabatiwa ukarabati wa Kampuni la Samsung  ya Shule ya Msingi ya Irmorijo Monduli Arusha ambapo Kammpuni ya Samsung ilitangaza kutoa msaada wa milioni 144 kwa shule hiyo na Sekondari ya Winning Spirit

No comments:

Post a Comment