Wednesday, August 15, 2012

SERGIO AGUERO AICHOKONOA MANCHESTER UNITED


LONDON, England

Aguero, aliyefunga mabao 30 katika msimu wake wa kwanza katika soka la England, anaamini nyota wa Man City wamethibitisha kuwa hawakamatiki katika mechi ya Ngao ya Jamii waliyoshinda dhidi ya Blues

SIKU chache kabla ya kuanza kwa smimu mpya wa Ligi Kuu ya England, mshambuliaji Sergio Aguero anaamini mabingwa watetezi wa ligi hiyo Manchester City, wako tayari kuzima matarajio ya majirani zao kwa mara nyingine.
Muargentina huyo alifunga dakika ya mwisho kuipa City ubingwa huo msimu uliopita, huku akizima matarajio ya mshambuliaji Wayne Rooney na kikosi chake caha Manchester United.
Na kuelekea pambano la juzi la Ngao ya Jamii kati ya City na Chelsea, Rooney aliyefunga jumla ya mabao 35 ya michuano ya ndani msimu uliopita alikaririwa akiionya City kuwa hatima ya mwisho ya ubingwa wa msimu huu iko mikononi mwa United.
Lakini Aguero, ambaye alifunga jumla ya mabao 30 katika msimu wake wa kwanza wa kuvutia katika soka la England, anaamini nyota wenza kikosini Etihad wamethibitisha uhatari wao katika mechi ya Ngao ya Jamii waliyoshinda dhidi ya Blues.
“Tumefanya mwamzo mwema wa msimu na wiki hii tunaingia katika mechi yetu ya kwanza ya utetezi wa taji letu.
“Tumeanza kupiga hatua juu ya wengine na tuna matumaini kuwa Mungu atataubaklisha katika kiwango na morali tuliyonayo kama hivi. Tumekuwa timu imara na tumeanza kuelewana zaidi ya ilivyokuwa.
“Tutajaribu kuanza kama ilivyokuwa msimu uliopita na kufanya mambo vema zaidi. Nimekuwa nikiomba na kujiona kama tunaoweza kufanya hivyo tena. Sitaki kusema kwamba msimu utakuwa rahisi, lakini tuna timu nzuri ya kufanya hivyo.”
Aguero alijiandikia jina katioka historia ya City, kufuatia bao tamu la dakika za majeruhi kuipa ushindi uliowatawaza mabingwa baada ya miaka 44 katika siku ya kufunga msimu dhidi ya QPR.
Lakini sasa Aguero anasisitiza kuwa, huo ulikuwa mwanzo tu: “Mimi nilielewa siku ya pili kile nilichofanya dhidi ya QPR. Lakini sasa kwambaaa nina imani kubwa na matumaini kuwa City inaweza kushinda zaidi,” alimaliza Aguero katika tambo zake.

No comments:

Post a Comment