Thursday, August 16, 2012

SKYLIGHT BAND YAINGIA KWA KISHINDO 'Joniko Flower' ndani


Mwimbaji wa Bendi Mpya ya Skylight, Sonny Masamba (wa pili kulia), akiwaongoza wenzake kuimba wakati wa kuitambulisha bendi hiyo katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam Agosti 15.2012. Bendi hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Skylight Entertainment itakuwa ikiporomosha muziki wake katika mahadhi ya Afropop. Kulia ni Meneja wa Bendi, Aneth Kushaba. 
*******************
Ndugu Wanahabari, tunapenda kuchukua fursa hii kuwashukuru kwa kuchukua muda wenu katika ratiba zenu ngumu za majukumu yenu kuja kusikiliza yale tuliyowaita kuwaeleza.

Kwa kupitia nyie ndugu zetu,tunaamini ujumbe wetu wa habari njema kwa wapenzi wa burudani nchini zitawafikia kwa haraka na urahisi.

Tunaomba rasmi ushirikiano  wenu katika jambo hili la juhudi zetu za kuleta mapinduzi ya kiburudani katika soko la Muziki wa Bendi Tanzania.

Tunafurahi kuwatangazia Umma wa watanzania wapenda burudani,hasa musiki wa bendi,kuwa SKYLIGHT ENTERTAINMENT COMPANY inawaletea bendi mpya ya mahadhi ya AFROPOP kwenye soko la burudani Tanzania.

Bendi yetu mpya ya Skylight imesheheni wanamziki bora na wenye vipaji vya juu na uzoefu mkubwa katika muziki wa hapa Tanzania na mataifa mbalimbali.Leo tumewaita ili tutambulishe rasmi bendi yetu kwenu na kuwajulisha kuhusu burudani kabambe itakayoletwa kwenu na squad hii kali.

Kuwatambulisha kwenu team nzima ya Skylight ni kama ifuatavyo: Kiongozi wa bendi (Band Manager ) ni Anneth Kushaba, Waimbaji: Anneth Kusheba(AK47), Joniko Flower, Sam Machozi, Sonny Masamba na Marry Lucas.

No comments:

Post a Comment