Thursday, August 16, 2012

TANGA WAKOMAA NA MAZOEZI YA NGUMI


 Bonzo(63yrs) akitoa nasaa baada ya kumpiga bondia chipukizi james martin(22)ambae ni sawa na mwanae wa tatu.upande wa kulia ni Ibrahim kamwe na kushoto ni Yasin Abdallah-Ustadh
Mohamed Bonzo(63) inasemekana ndio bondia mzee nchini atacheza siku ya iddi mosi.

Kampuni  ya  Mwanzoa Promotions ya Tanga chini ya mkurugenzi wake Ally  Ommar inaendeleza mkakati wake wa kunyanyua vipaji vya wanamichezo wa jiji la Tanga hasa katika mchezo wa ngumi kwa mapambano ya ubingwa wa Afrika mashariki yatakayopigwa siku ya iddi mosi na iddi pili. 

Ally omar’Mwazoa’ akikimuhakikishia katibu mkuu wa ngumi za kulipwa nchini Ibrahim kamwe”bigright” kuwa maandalizi ya mapambano yote yamekamilika na mabondia  wapo katika hali nzuri ya ushindani ambapo siku hiyo ya iddi mosi katika ukumbi wa CCM HALL, Said mundi wa Tanga atazipiga na Habibu pengo wa Dar es salaam.

Katika kugombania ubingwa wa Taifa wa TPBC uzito wa super feather raundi kumi,nae jumanne Mohamed wa Tanga atazipiga na ali bugingo wa Dar es salaam uzito wa light weight raundi kumi,katika uzito wa super fly Haji juma(Tanga) na Mwaite juma(Dsm) watacheza raundi nane na mapambano mengineyo mengi ya utangulizi wa mabondia wa watakaotoka katika vitongoji mbalimbali vya jiji la tanga.
 
Na siku ya idi pili katika ukumbi wa pweza kutakuwa na pambano kubwa la ubingwa wa Afrika mashariki na kati, kati ya Alen Kamote wa Tanga na bondia toka Uganda ni pambano la raundi kumi pia zuberi kitandula wa Tanga atazipiga na Sadiki Abdul azizi wa Dar es salaam raundi kumi,jay jay ngotiko wa tanga atapigana na bondia juma afande toka morogoro pia kutakuwepo na mapambano mengi ya utangulizi ya mabondia wakongwe wa tanga na wale chipukizi takribani mabondia wote wa kulipwa wa jiji la Tanga watashindana hakuna atakaekosa kazi labda awe na matatizo binafsi. mwazoa alimalizia kwa kusema hizi ni mbio za kuyakusanya mataji yote ya Tanzania na Afrika mashariki yaje mkoani Tanga na tayari mpaka sasa ina mabingwa sita wa Tanzania na mmoja wa Afrika mashariki.

No comments:

Post a Comment