Saturday, September 22, 2012

‘APATE RAHA’ YA SUMA LEE HIYOOO RUNINGANI



Na Elizabeth John
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ismail Seif  ‘Suma Lee’ ameachia video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Apate raha’ ambao unafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Suma Lee alisema video ya wimbo huo imeanza kuonekana hivi karibuni na ana uhakika utafanya vizuri kutokana na mandhari aliyotumia katika kuitengeza video hiyo.
“Namshukuru Mungu kazi zangu huwa zinapokelewa vizuri na mashabiki wangu, kitu ambacho kinanipa morali ya kuendelea kufanya kazi,” alisema Suma Lee.
Suma Lee akawaomba mashabiki wake waendelee kumpa sapoti katika kazi zake na kwamba wasicheze mbali na yeye kuna vitu vingi vizuri ambavyo amewaandalia.
Ukiondoa kibao kipya cha Apate raha, Suma Lee aanaendelea kukumbukwa kwa vibao vyake vingine kama, Chungwa, Hakunaga, Asiyecheza atoke na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini kwa nyakati tofauti.

No comments:

Post a Comment