Tuesday, September 25, 2012

BARNABA: 'SIJUTII KWA ALIYEKUWA NAYE' INAKUJA KUWASHIKA



Na Elizabeth John
MSANII wa muziki wa Kizazi Kipya nchini, Barnabas Elias ‘Barnaba,’ anajiandaa kuachia 'pini' jipya aliyoipa jina la 'Sijutii kwa niliye kuwa naye.'
Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam leo, Barnaba alisema yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa song hilo ambalo anaamini litafanya vizuri kutokana uwezo alionao katika tasnia ya muziki.
“Kama kawaida yangu nyimbo zangu nyingi huwa haziwachukizi mashabiki, ni jambo ambalo namshukuru Mungu, kwani ni wasanii wachache ambao nyimbo zao zinafanya vizuri mtaani kiasi hicho,” alisema.
Barnaba alisema anaamini 'Sijutii kwaniliye kuwa naye' kitafuata nyayoz ya vibao vyake vilivyotangualia, na kwamba kwa sasa yupo katika mchakato wa kutafuta mrembo ambae atapamba video ya kazi hiyo.
Mkali huyo amewaomba mashabiki wa muziki nchini kukaa mkao wa kula kukipokea kibao hicho.
Mbali na kibao hicho, Barnaba aanakumbukwa kwa makali yake aliyoyaonesha katika vibao vyake kama, Magubegube, Wrong number, Tulizana, Milele Daima na nyinginezo ambazo zinafanya vizuri katika tasnia ya muziki wa Kizazi Kipya nchini.

No comments:

Post a Comment