Friday, September 7, 2012

FFU WAZIDI KUWAPAGAWISHA WATASHA KATIKA JUKWAA LA ALAFIA FESTIVAL 2012 HUMBURG, UJERUMANI


* FFU Ngoma Africa Band, Ughaibuni wafunika tena Alafia Festival,Hamburg

Wiki iliyopita Siku ya Jumapili 26.08.2012 katika maonyesho ya Alafia Festival,mjini Hamburg, Ujeruman, Kikosi cha Ngoma Afrika band aka FFU,kiliwasha moto na kuwapagawisha vilivyo mashabiki wake na watasha kibao waliofurika katika Tamasha hilo la Alafia Festival, kwa miondoko yake.

Bendi hiyo maarufu  ya muziki wa dansi barani ulaya ilikuwa na kazi moja tu ya kuwadatisha vilivyo mashabiiki
katika onyesho hilo la Alafia mjini hamburg.

Mashabiki wengi wa bendi hiyo walijikuta wakidatishwa akili na mdundo na miondoko ya FFU.

Ngoma Africa band wanashikilia Tuzo ya kimataifa ya IDA-International Diaspora Award, pia wanatamba na CD mpya Bongo Tambarare, wasikilize at www.ngoma-africa.com

No comments:

Post a Comment