Saturday, September 1, 2012

JWTZ MORO WAADHIMISHO MIAKA 48 KWA KUFANYA USAFI WA NGUVU KATIKA SOKO KUU LA MKOA.



Sehemu ya askari wa jeshi la wananchi la kujenga taifa (JWTZ) kutoka shule ya mafunzo na huduma Pangawe Morogoro wakieka takangumu katika lori wakati wa zoezi la kufanya usafi ndani na nje ya soko kuu la mkoa huo ikiwa ni sehemu mojawapo ya kuadhimisha maadhimisho ya miaka 48 tangu kuanzisha kwa jeshi hilo ambapo kilele cheke hufanyika kila septemba mosi kila mwaka hapa nchini.
Hapa askari hao wakiwa na tenga lenye uchafu wakielekea katika lori kwa ajili ya kutupa taka hizo.
Wakikusanya uchafu uliopo chini na kuweka katika vyombo.
Kazi hiyo iliendelea katika sehemu nyingine katika soko hilo kama wanavyoonekana askari hao wakiendelea na zoezi hilo.
Askari huyu akizoa takangumu kutoka chini na kuweka katika toroli baada ya kuutoa ndani ya mtaro katika mtaa wa Uhuru unaopakana na soko kuu hilo.
Kwa kweli kazi zilikuwa nyingi sana hapa afande akisukuma toroli lenye taka hizo wakati akielekea kwenye lori.

SHULE ya huduma na mafunzo ya jeshi la wananchi la kujengataifa (JWTZ) Pangawemkoa wa Morogoro inatarajia kuadhimisha miaka 48 kwa kufanya michezo mbalimbali wakati wa kilele chicho itayofanyika kwenye viwanja vya shule hiyo kesho mkoani hapa.

Akizungumza na gazeti hili mjinihapa Afisa Mahusiano wa shule hiyo Meja Henry Komba alisema kuwa jeshi hilolinatarajia kuadhimisha miaka 48 tangu kuundwa kwake kwa kufanya michezo ainasita kwa wanamichezo kushiriki michezo hiyo.

Komba alisema kuwa michezo hiyoni pamoja na soka, netiboli, wavu, kukimbiza kuku, kuvuta kamba, wavu na mashindano ya kwata.

“Tunaanzimisha miaka ya 48 tangu kuundwa kwa  JWTZ na kilele chake hufanyika kila septemba 1 na mwaka huu uongozi wa Pangawe tumefanya kazi tatu za kijamii katika maeneo matatu tofauti kwa kufanya usafi katika soko kuu la mkoa wa Morogoro, kuchangia damu katika benki ya damu hospitali ya rufaa ya mkoa na kufanya pia katika kituo cha Mgolele Bigwa” alisema Komba.

Alitaja kazi ambazo wamefanyakakuwa ni  pamoja na kufanya usafi katikakituo cha kulelea watoto yatima cha Mgolole kilichopo Bigwa, kuchangia damukatika benki ya dawa ya hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro na kufanya usafindani na nje ya soko kuu la mkoa huo.

Akieleza juu ya michezo hiyoKomba alisema kuwa askari wenye umri mkubwa watahusika na  michezo miwili ya kuvuta kamba na kukimbizakuku wakati vijana wa kiume wao watashindana katika mchezo wa soka hukuwasichana wakionyeshana ubabe katika mchezo wa netiboli na mchezo wa wavu.

Aliendelea kueleza kuwa katikamashindano ya kwata itajumuisha kombania aina mbalimbali na michezo hiyoinatarajia kuanza majira ya saa 2 asubuhi na kumalizika majira ya saa 7 mchana.

Komba alisema kuwa baada yakumalizika kwa michezo hiyo kutakuwa na hafla itayowakutanisha askari wotewakiwemo na maafisa wa jeshi hilo.

No comments:

Post a Comment