SACCO - Yapatiwa Mkopo Wa Matrekta Na Benki Ya Raslimali-TIB
Matrekta 11 yaliyotolewa mkopo kwa wanachama wa Talanta SACCOS ya tarafa ya Kinyangiri wilaya ya Mkalama Mkoani Singida.
Mkuu
wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone, akizungumza na wananchi kisha
alikabidhi matrekta makubwa 11 kwa wanachama wa Talanta SACCOS ya tarafa
ya Kinyangiri wilaya Mkalama, yaliyotolewa mkopo na Benki ya rasilimali
(TIB), kwa gharama ya Sh.Milioni 450.5.
Mwenyekiti
wa Talanta SACCOS tarafa ya Kinyangiri Mayasa Salum,akifurahia trekta
alilokopeshwa na benki ya rasilimali (TIB), kupitia SACCOS hiyo.
MKUU
wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Kone akikaribishwa na mmoja wa wanachama
wa ‘Talanta SACCOS’ katika kijiji cha Iguguno tarafa ya Kinyangiri
wilaya ya Mkalama alipoenda kukabidhi matrekta 11 yaliyogharimu Sh.
Milioni 450.5.
Na: Elisante John,Singida
Wananchi
wametakiwa kujiunga katika vikundi ili kunufaika na mikopo inayotolewa
nataasisi za vyombo vya kifedha. Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Kone,alisema
hayo wakati wa kukabidhi matrekta makubwa 11 kwa Talanta SACCOS ya
tarafa ya Kinyangiri, wilayani Mkalama, yenye thamani ya Sh. Milioni
450.5 kutoka benki ya raslimali (TIB). Dk. Kone alisema kupitia ushirika
wakulima na wananchi kwa ujumla watanufaika na mkakati wa kilimo
kwanza.Kwa upande wake mwenyekiti wa Talanta SACCOS, Myasa Salum
aliishukru benki hiyo ambayo imelenga kumkomboa mkulima wa kawaida
kijijini.
No comments:
Post a Comment