Tuesday, September 25, 2012

KAMPUNI YA KUSAFIRISHA MIZIGO YA SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD YAKABIDHI MSAADA WA VITU MBALIMBALI VILIVYOTOLEWA NA WATANZANIA WAISHIO UINGEREZA KUWASAIDIA WAKAZI WA MABWEPANDE


Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam  Saidi Meck Sadiki (kulia) akipokea msaada wa vitu mbalimbali vilivyotolewa na watanzania waishio nchini Uingereza kuwasaidia wakazi wa Mabwepande walioathiriwa na mafuriko yaliyotokea mwezi Desemba 2011 jijini Dar es salaam leo. Wanaokabidhi msaada huo ni kutoka kushoto ni Awadh Salim mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Bw. Mohammed Abdulrahaman Meneja wa kampuni hiyo Tanzania na Bw. Chris  Lukosi, Mkurugenzi wa  Kampuni ya Usafrishaji wa Mizigo ya Serengeti.

Mkurugenzi wa  Kampuni ya Usafrishaji wa Mizigo ya Serengeti (Serengeti Freight Forwarders Ltd) Bw. Chris Lukosi akimkabidhi  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam  Saidi Meck Sadiki (kulia) moja ya boksi lenye vitu mbalimbali vilivyotolewa na watanzania waishio nchini Uingereza kuwasaidia wakazi wa Mabwepande walioathiriwa na mafuriko yaliyotokea mwezi Desemba 2011 jijini Dar es salaam.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam akiwaeleza jambo viongozi wa Kampuni ya Usafirishaji wa Mizigo ya Serengeti (Serengeti Freight Forwarders Ltd) iliyosafirisha bure msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo viatu, nguo na vifaa vya watoto vilivyotolewa na watanzania waishio nchini Uingereza kuwasaidia wakazi wa mabwepande.

No comments:

Post a Comment