Saturday, September 8, 2012

KUELEKEA BRAZIL 2014; ENGLAND, UJERUMANI, UHOLANZI ZATISHA, ITALIA YABANWA


Mshambuliaji wa England Jermain Defoe (katika) akifumua shuti kufunga bao la tatu la timu yake dhidi ya Moldova kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2014. England ilishinda 5-0

LONDON, England

Makocha wawili raia wa Italia nao pia walikuwa na usiku bora zaidi baada ya kuziwezesha timu zao kushinda, ambao ni Fabio Capello na Giovanni Trapattoni, wanaozinoa timu za taifa za Russia na Ireland

TIMU za taifa za England, Ujerumani, Ufaransa na Uholanzi, zimeanza vema harakati zake katikia safari ya kutinga fainali za Kombe la Dunia 2014 zitakazofanyika nchini Brazil, lakini Italia ikajikuta ikizua maswali katika mechi za kuwania kufuzu kutokea bara la Ulaya Ijumaa usiku.

Mabingwa wa dunia Hispania waliokuwa wakicheza kirafiki na kushinda mabao 5-0 dhidi ya Saudi Arabia, watafungua harakati zao katika hatua hii Jumanne, lakini Wataliano Azzurri wakamaliza dakika 90 kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Bulgaria katika kundi la B.

England kwa upande wao walikuwa na ufunguzi wa kuvutia katika kundi la H, baada ya kuibuka na ushindi wa mbaoa 5-0 dhidi ya Moldova, usiku ambao Ujerumani nayo ilitoka kifua mbele kwa mabao 3-0 dhidi ya Visiwa vya Faroe katika kundi la C.

Bao la kipindi cha kwanza la Abou Diaby liliipa Ufaransa ushindi wa bao 1-0 katika kundi I dhidi ya wenyeji wao Finland, huku Uholanzi ikiichapa Uturuki kwa mabao 2-0, shukrani kwa mabao ya Robin van Persie na Luciano Narsingh katika mechi ya kundi D jijini Amsterdam.

Italia mabingwa mara nne wa Kombe la Dunia, walishindwa kutoka na ushindi katika jiji la Sofia na kujikuta ikimaliza sare ya 2-2 dhidi ya wenyeji wao Bulgaria, ambapo Pablo Osvaldo alifunga mabao yote na Azzurri kuongoza mechi kwa 2-1 baada ya kuwa ilisharuhusu bao moja.

Georgi Milanov akawasawazishia wenyeji hao na kuipoka Italia ushindi muhimu katika harakati za kuelekea Brazil.

Makocha wawili raia wa Italia walikuwa na usiku bora zaidi baada ya kuziwezesha timu zao kushinda, ambao ni Fabio Capello na Giovanni Trapattoni, wanaozinoa timu za taifa za Russia na Ireland.

Ireland ilizindua vema jaribio la kutinga fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 2002 ilipofungua pazia lake kwa ushindi wa mabao yaliyowekwa nyavuni na Robbie Keane, kukipa kikosi cha Trapattoni ushindi wa 2-1 dhidi ya Kazakhstan katika kundi la C.

Russia inayonolewa na Capello aliyeachia ngazi kuinoa England, iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ireland ya Kaskazini, shukrani kwa mabao ya Viktor Faizulin na Roman Shirokov, kwenye pambano kali jijini Moscow.

Ushindi mkubwa zaidi katika mechi za juzi kufuzu Brazil 2014, ni ule wa Bosnia, iliyoshinda kwa mabao 8-1 dhidi ya Liechtenstein, Edin Dzeko akifunga matatu ‘hat-trick’ na kuweka rekodi ya kuwa nyota aliyefunga mabao mengi zaidi (25) timu ya taifa – hiyo ikiwa ni mechi ya kundi la G.

1 comment:

  1. When I origіnally commented I clіcked the "Notify me when new comments are added" chеckbox and now eаch tіmе a comment іs аdԁed I get four emails with the same
    comment. Is there any way you can remove me from that ѕervice?
    Bless you!

    Feel free to ѵisit my site; 24 hour Plumber Solihull

    ReplyDelete