Saturday, September 8, 2012

ROONEY: NITAKAA MANCHESTER UNITED KWA MIAKA 10 IJAYO


MANCHESTER, England

“Matumaini yangu ni kwamba nitakuwa hapa kwa muda mrefu. Hii ni klabu kubwa na acha niwe mwaminifu, hivi unaweza kutamani kutoka katika klabu kama hii? Imekuwa ni timu kubwa duniani”

MSHAMBULIAJI Wayne Rooney juzi usiku amevunja ukimya na kuimbia klabu yake ya Manchester United kuwa yeye anatarajia kukaa kwa muda mrefu klabu Old Trafford, kama anavyotaka mwenyewe.

Rooney nyota wa kimataifa wa England, amekuwa na mwanzo mbaya wa msimu klabuni hapo na kuzua maswali, ikidaiwa kuwa ana mahusiano mabaya na bosi wake Mskochi Sir Alex Ferguson.

Mkali huyo kwa sasa anaguguza jeraha la kuchanika juu ya goti lake kutokana na kuchimbwa na daruga la nyota wa Fulham Hugo Rodallega na yuko nje ya dimba kwa miezi miwili, akitakiwa kurejea kupigania namba pindi atakapopona.

Lakini juzi usiku Rooney, 26, akasema anajisikia furaha kuwa sehemu ya kikosi chake na kwamba anakusudia kuhitimisha zama zake dimbani akiwa na United, akisisitiza kuwa analeta kuwa na muongo mmoja wa aina yake akiwa na Mashetani Wekundu hao.

Shujaa huyo wa zamani wa klabu ya Everton, alisema: “Naweza kuwa hapa kwa miaka mingine 10? Natumaini itakuwa hivyo. Kama nilivyopania kwa muda mrefu kuwa hapa, kisha na nikawa hatimaye mchezaji wa Manchester United.

“Ni wazi kwamba nilikumbana na hali ngumu hapa miaka michache iliyopita, lakini nikaweka wazi haraka sana kuwa nilifanya makosa. Kama muda mrefu watu wanavyotaka mimi kuwa mchezaji wa United, basio ndivyo nitakavyokuwa.

“Matumaini yangu ni kwamba nitakuwa hapa kwa muda mrefu. Hii ni klabu kubwa na acha niwe mwaminifu, hivi unaweza kutamani kutoka katika klabu kama hii? Imekuwa ni timu kubwa duniani,” alisisitiza Rooney.

Rooney akaongeza kuwa anahitaji kuangalia kila pande ya chumba cha kuvalia cha klabu yake ya kuona ni namna gani anaweza kuboresha kazi akiwa na United kwa muda mrefu kadri iwezekanavyo.

Akasema: “Unapaswa tu kuwaangalia nyota kama Ryan Giggs na Paul Scholes na namna walivyopata mafanikio, wao ni mfano wa kuigwa nasi sote. Hilo ndilo wazo na mpango wangu na nina matumaini itakuwa hivyo pia,” alimaliza Rooney

No comments:

Post a Comment