Saturday, September 8, 2012

SERENA WILLIAMS, VICTORIA AZARENKA FAINALI US OPEN KESHO



NEW YORK, Marekani

MMAREKANI Serena Williams amefanikiwa kumtupa nje ya Michuano ya Wazi ya Marekani ‘US Open 2012’ nyota wa Italia Sara Errani kwa ushindi wa seti mbili za 6-1 6-2 na kutinga fainali yake ya sita ya mashindano hayo, na kesho anaumana fainali Victoria Azarenka.

Serena bingwa mara 14 wa Grand Slam, ambaye alijishindia dhahabu ya Olimpiki 2012 jijini London, alilazimika kutumia muda wa takribani dakika 64 kumshinda Errani anayeshika nafasi ya kumi ya viwango vya ubora dunia, katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Arthur Ashe.

Kwa ushindi wa juzi, Serena ameendelea kuongeza uidadi ya mechi za kushinda, ambapo amepoteza mechi moja tu kati ya 26 alizocheza tangu alipoangukia pua katika raubndi ya kwanza ya Michuano ya Wazi ya Ufaransa ‘French Open’ Mei 29.

Fainali ya leo inamrudisha Serena dimbani akipania kushinda ubingwa wa nne jijini hapa dhidi ya Azarenka, raia wa Belarus aliyefanya kazi ya ziada kumchapa Maria Sharapova katika nusu fainali ya kwanza Ijumaa.

Akizungumzia ushindi huo, Serena alisema: "Imekuwa ajabu sana kurudi tena katika fainali hii tena. Niliota kuhusu hili kwa mwaka mzima na kimsingi kweli nina furaha kubwa.

"Itakuwa furaha kuu kushinda tena ubingwa wa US Open, lakini Victoria (Azarenka) anahitaji pia kuutwaa. Napenda kucheza hapa. Daima ni heshima na furaha kama hiyo," alisema Serena kwa furaha baada ya ushindi wake dhidi ya Errani juzi Ijumaa.

1 comment:

  1. Spend your time and energy out of your day job
    doing fun activities you're keen on in order to make the extra cash your allowance will cherish. In general, the payday advances can extend to time of an fortnight however, many extend the loans around 18 days.

    my web site; advance cash

    ReplyDelete